• Elius' Letters
  • Posts
  • Jinsi Mjasi wa Tanzania Anavyotumia AI Kupata Wateja Kupitia Social Media

Jinsi Mjasi wa Tanzania Anavyotumia AI Kupata Wateja Kupitia Social Media

Wanakuambia "tengeneza personal Brand" na unabaki unashangaa personal brand ni nini na naweza kuibuild vipi ukiwa na simu moja na bundle ya wiki.

Jinsi Mjasi wa Tanzania Anavyotumia AI Kupata Wateja Kupitia Social Media

Leo nakuelezea full framework jinsi navyotumia AI kuuza Online, in one letter.

Karibu

Habari ndugu yangu. McBenvics hapa.

Umejiandikisha kupata barua zangu kila week, na mimi nimeahidi kukupa. Hii hapa ya leo. Sio video ya masaa matatu, sio course ya wiki nzima. Ni barua moja ndefu, umeketi na chai au kahawa, unasoma mara moja, unachukua kile kinachokufaa.

Nimeandika hii kwa sababu nimeona kitu kinakera kwenye soko letu. Wajasi wengi Tanzania wanafanya kazi kubwa kwenye Instagram, TikTok, WhatsApp, lakini gap kati ya "naposti content" na "napata wateja" ni kubwa kuliko mtu yeyote anavyokwambia. Watu wanakuuzia tools, wanakuuzia courses, wanakuuzia mindset. Hakuna anayekwambia mfumo halisi wa namna AI inavyoweza kuingia kwenye biashara yako leo, kwa lugha unayoielewa, na kwa hali halisi ya soko la Tanzania.

Hii ndio nimekuandikia. Soma polepole. Hakuna haraka.
Mjasi ni mjasiliamali anayetumia technolojia na Social media kufanya kazi zake… mimi na wewe.

The Mjasi problem

Hebu niseme kitu ambacho nimegundua baada ya kukutana na Wajasi wengi mwaka huu.

Watu wengi wanafikiri tatizo lao ni content. "Sijui nipost nini." "Sijui ni-record nini." wengine wanasema "Algorithm imenikataa." Lakini ukikaa nao na kuuliza maswali, unagundua tatizo halisi sio content. Tatizo ni kwamba content inafanya kazi yake, wateja wana-DM, watu wanaco-mment, watu wanauliza bei, lakini baada ya hapo kila kitu kinaanguka. Mjasi anachoka. Anasahau ku-reply. Ana-reply baada ya siku tatu wakati mteja ameshapoa. Au una-reply, lakini hujui nini cha kusema baada ya "bei ni elfu thelathini."

Hii ndio gap nalozungumzia. Sio kuonekana wala kufikia watu wengi. Ni kile kinachofuata baada ya visibility kufanya kazi yake.

Na hapo ndipo wengi wanakwama. Kwa sababu kupata views unaweza kujifunza kutoka kwa creator yeyote kwenye Instagram. Lakini kile kinachofuata, tunakiita “conversion,” hakuna mtu anakufundisha kwa lugha rahisi. Wanakuambia "tengeneza personal Brand" na unabaki unashangaa personal brand ni nini na naweza kuibuild vipi ukiwa na simu moja na bundle ya wiki.

Nakwambia, hii ni reality na ni muhimu tuizungumzie. Na ndio sababu nimekuandikia.

What changes when you put AI in the loop

Nimegundua kitu rahisi sana. AI haifanyi miujiza. AI inachofanya ni kuchukua kazi mbili ambazo Mjasi anazifanya kila siku, na kuzifanya zifanyike kwa kasi, kwa ubora, na bila wewe kuchoka.

  1. Kazi ya kwanza ni kufikiri. Kufikiri ni-post nini. Kufikiri nijibu vipi wateja. Kufikiri nipackage vipi offer yangu. Kazi hii inachukua muda mwingi sana, na ndio sababu Mjasi anakaa wiki nzima bila kupost kitu chochote. Si kwa sababu hana kitu cha kusema. Ni kwa sababu kufikiri kunachosha.

  2. Kazi ya pili ni kushughulikia kile kinachojirudia. Mtu ame-DM, una-reply nini. Mtu ameuliza bei, una-explain vipi. Mtu amesema "nitafikiri" na hakurudi tena, una-follow up vipi bila kuonekana mwenye njaa. Kazi hii ni endelevu, haina mwisho, na ndio inayowachosha Wajasi zaidi ya kitu kingine chochote.

AI inakuja kwenye kazi hizi mbili. Sio kuzifanya badala yako. Inakuja kama mshirika ambaye unaweza kumwambia "nisaidie kufikiri hii" au "nisaidie kuandika hii" na anakurudishia kitu unachoweza kuki-edit, kuki-tumia, kukipeleka kwa wateja na kuuza kabisa. Yeye ndiye anayekupa draft ya kwanza. Wewe unabaki kuwa mtu wa maamuzi ya mwisho.

Hii ndio loop. Visibility (Kuonekana aka Kupata views), conversation (Mazungumzo), conversion (Kununua), kurudia (Kuwa mteja wa kudumu). Na kila hatua kwenye loop, AI inaweza kuingia kama mshirika sio mbadala. Hii ni tofauti muhimu uielewe. Mjasi anayefikiri AI itamreplace anaishia kupata content zinazokaa kama robot kabisa. Mjasi anayetumia AI kama mshirika anaishia kupata content inayoongea kama yeye mwenyewe lakini zinakuwa zimewekewa mawazo mazuri zaidi.

Sasa ngoja nikuonyeshe mfumo kabisa, au unasemaje.

The system, in concrete steps

Hatua ya kwanza ni kuelewa wateja wako kuliko unavyowaelewa sasa hivi. Hii ni hatua ambayo Wajasi wengi wanairuka kwa sababu inaonekana ya theoretical sana. Lakini hapa ndipo kila kitu kingine kinaanzia. Biashara yako online haiwezi kutoboa kabisa kama hujawaelewa wateja wako kwa level ya juu. Tafadhali naomba urudie kusoma hii paragraph.

Chukua AI yako, yoyote unayotumia, ChatGPT au Claude au nyingine. Mwambie hivi.

"Mimi nina biashara ya [taja biashara yako kama ambavyo ungenielezea mimi]. Wateja wangu wakubwa ni watu wa aina gani? Wanafikiria nini wanapokuwa wanatafuta kitu kama changu? Ni maneno gani wanayotumia kuongelea tatizo lao kabla hawajajua suluhisho lipo?" 

Kisha mpe context au maelezo kidogo kuhusu wateja watatu au wanne ambao tayari umeshakuwa nao. Hapa siongelei data za kifedha wala takwimu. Mpe maelezo halisi kabisa ya watu halisi. AI itakurudishia uchambuzi ambao unaweza kuushangaa, kwa sababu mara nyingi tunachowadhania wateja wetu wanafikiri ni tofauti kabisa na kile wanachofikiri kweli.

Hatua ya pili ni kuandika content inayowavuta watu wanaofanana na wateja wako bora, sio watu wote. Hapa ndipo Wajasi wengi wanapotea. Wanaandika content generic kwa sababu wanaogopa kupoteza watu. Lakini content generic haivutii mtu yeyote.

Mwambie AI yako,

"Kwa msingi wa watu hawa niliokuelezea, andika ideas tano za posts ambazo zitawagusa watu kama hao moja kwa moja. Nataka post zinazoongea na mtu mmoja sio kundi la watu." 

Halafu chukua hizo ideas, ziangalie, choose moja feel true kabisa kwako, na uiandike kwa sauti yako mwenyewe. AI inakupa muundo. Wewe unaipa roho. Ukiona AI imekosea usiiopotezee kabisa na kudhani “basi ai haiko vizuri”, kuwa patient.

Hatua ya tatu ni kushughulikia DMs na WhatsApp messages bila kuchoka.

Hapa ndipo AI inakuwa muhimu zaidi. Tengeneza document moja, andika maswali yote ambayo watu wanakuuliza mara kwa mara kuhusu biashara yako. Bei. Delivery. Process. Tofauti kati ya offer moja na nyingine. Andika majibu yako bora kwa kila swali, kwa sauti yako. Hii ni one-time work, unaifanya mara moja ndani ya masaa mawili au matatu. Baadaye, kila mtu anayeku-DM, unaweza kutumia AI kukusaidia kuandika reply fasta kwa sababu AI tayari ina-context ya majibu yako bora. Wewe haupotezi sauti yako. Unapata speed tu. Na pesa inapenda Speed.

Hatua ya nne ni follow-up.

Hii ni hatua ambayo wengi wanairukaga, na ndio inayopoteza wateja zaidi. Watu wengi wanauliza bei au kama product ipo, unawajibu, hawajibu, na wewe unawasahau. AI inaweza kukusaidia kuwafuatilia. Sio kwa kuandika messages za ovyo hapana, Kwa kukukumbusha tu. AI atakwambia "Mtu huyu ameDM siku tatu zilizopita, alikuwa anauliza kuhusu offer yako, hujamjibu kwa undani. Hapa kuna pendekezo la message ya follow-up kwa sauti yako." Wewe unachukua hyo message unaiedit, unaiuma, na mteja anarudi.

Hatua ya tano ni kujifunza kutokana na kile kinachofanya kazi.

Kila wiki, chukua dakika thelathini, fungua AI yako, na mwambie

"Hizi ndio posts zilizoperform vizuri wiki hii. Hizi ndio zilizofanya vibaya. Unaona pattern gani? Nifanye nini tofauti wiki ijayo?"

Sasa hapa nataka unisikilize kwa Umakini Mjasi, hapa AI haitakupa jibu kamili. Lakini itakupa pattern ambazo wewe peke yako ungeshindwa kuona kwa sababu uko karibu sana na content yako mwenyewe.
Hii ndio loop nzima. Visibility inayolenga watu sahihi ili kila views ziwe na maana, conversation, mazungumzo yanayotunzwa, conversion inayofuatiliwa kwa follow up, na kujifunza kunakoendelea. Hakuna sehemu yoyote ya huu mfumo inahitaji budget kubwa. Inahitaji uamuzi wa kufanya kazi kwa namna mpya, kwa kutumia AI.

Niseme kitu kingine hapa. Baada ya kufanya kazi hii kwa mwenyewe kwa wateja wangu wa kwanza, niligundua kwamba sehemu ya tatu, kushughulikia DMs na WhatsApp, ndio inayotumia muda mwingi zaidi. Ndio sababu nimejenga mfumo unaoitwa ARIA (AI Responsive Intelligence Assistant), ambao unafanya hatua hii iwe automated kwenye WhatsApp moja kwa moja hasa kwa Wajasi wenye mzigo mkubwa wa messages. Sio kila mtu anauhitaji. Mfumo huu ni wa watu walio kwenye stage ambapo mikono peke yake haitoshi. Lakini nakuelezea kwa sababu ni mfano wa namna hatua hizi zinavyoanza kwa kufanya mwenyewe kwa mikono na baadae zinavyoweza kukua kuwa system halisi kadri unavyokua.

The honest part

Lazima nikuambie kitu ambacho watu wengi hawatakuambia.

AI haitakuokoa kama biashara yako haina msingi, huu ni Ukweli na ikiwezekana isome tena hyo sentensi. Kama hujajua wateja wako ni nani, AI itakusaidia kuandika content vizuri zaidi lakini bado haitaleta wateja sahihi. Kama offer yako haijielezei wazi kabisa, AI itakusaidia kuiandika kwa maneno mazuri lakini bado haitanunuliwa. Kama huna uvumilivu wa kufanya kazi kwa mwezi mmoja bila kuona matokeo makubwa, AI haitakupa shortcut. This is the reality.

AI ni amplifier. Inakuza kile ulichonacho tayari. Kama una msingi mzuri, inakuza ubora. Kama una msingi mbovu, inakuza ubovu kwa kasi zaidi.

Hii ndio sababu sipendi kuuza AI kama suluhisho la kila kitu. Ni leverage. Ni chombo. Chombo kizuri sana. Lakini chombo kinahitaji mkono unaofahamu kazi. Na kazi unayoifanya wewe Mjasi, AI haiwezi kuifanya kwa niaba yako. Inaweza kukusaidia ndiyo lakini haiwezi kuireplace.

Kama umesoma hadi hapa na unaona kabisa nazungumza na wewe, basi uko mahali sahihi. Hii barua haijaandikwa kwa watu wanaotafuta miujiza. Imeandikwa kwa Wajasi wanaoelewa kwamba kazi ni kazi, na wanataka mfumo wa kuifanya kazi hiyo iwe na maana zaidi.

What happens next

Barua ya Elius' Letters inakuja kila ijumaa. Baada ya hapo, kila wiki, utapata barua mpya kutoka kwangu. Sio kila siku. Kila wiki, kwa sababu ndio speed ninayoweza kukutumia hizi barua bila kupoteza ubora. Naheshimu muda wako sana kuliko kukupa kitu cha kusoma kila siku ambacho hakijawekewa fikra zangu.

Halafu kuna kitu kingine ninachotaka kukuambia. Kama umesoma hii barua na unahisi unataka kufanya kazi hii pamoja na watu wengine, sio peke yako, huwa siko ofsini lakini huwa ninakaa ndani ya Zillim Growth Club. Hapo ndipo ninaspend muda wangu na Wajasi kila wiki, tunakaa, tunafanya kazi, tunashare majibu, tunajifunza kutoka kwa kila mmoja. Sio course (japo kuwa course zipo nyingi). Sio mafunzo tu. Ni mahali. Ni meeting point. Watu wanaokuja huku wanakuja kwa sababu wanataka kufanya kazi na watu wengine wanaofanya kazi.

Link iko hapa kama unataka kujiunga: https://www.skool.com/zillim-club-1340/about

Sio lazima ujiunge sasa. Soma barua zangu kwanza. Niangalie. Ona kama sauti yangu na fikra zangu zinakufaa. Halafu kama siku moja unahisi unataka kuja karibu zaidi, mlango uko wazi.

Asante kwa kusoma hadi hapa, ndugu yangu. Tutaonana kwenye barua inayofuata

McBenvics

Reply

or to participate.