- Elius' Letters
- Posts
- Ifanye ChatGPT iwe Partner wa Kufikiri, sio Chatbot ya kukusifia na Kukuabudu
Ifanye ChatGPT iwe Partner wa Kufikiri, sio Chatbot ya kukusifia na Kukuabudu
Mara ya mwisho ulipouliza ChatGPT iangalie wazo lako la biashara, ilikujibuje?
Nafahamu. Ilikuambia wazo ni kubwa sana. Ilikupa sababu kumi kwa nini utafanikiwa. Ilipendekeza frameworks. Ilimalizia kwa "let me know if you need anything else!"
Ulijisikia vizuri. Ulifunga laptop ukiwa na imani zaidi. Ukaendelea na siku yako.
Na hii ndio tatizo.
Kwa Nini ChatGPT Inakudanganya
ChatGPT haijengwi iwe mfikiriaji mnyoofu. Imejengwa iwe msaidizi wa kukupendeza na kukufurahisha. Tofauti kati ya hizi mbili ni kubwa kuliko unavyofikiri.
Msaidizi wa kupendeza anataka uendelee kuongea naye. Msaidizi wa kupendeza hatawahi kukuambia "wazo lako halina mwelekeo" kwa sababu hiyo inaweza kukufanya ukaache kutumia app yake. Msaidizi wa kupendeza atakubaliana na wewe kwa sababu hiyo ndiyo njia ya kukufanya ubaki.
Kwa burudani, hii ni sawa. Ukitaka ChatGPT ikusimulie hadithi au ikutengenezee ujumbe wa kuwatumia maharusi, hakuna shida.
Kwa biashara, hii ni hatari.
Unapoamua kuongeza bei. Unapoamua kuingia soko jipya. Unapoandika caption ambayo itaonekana na maelfu ya watu. Unapopanga offer mpya. Kwenye maamuzi haya, hutaki mshauri wa kukupigia makofi. Unataka mtu atakayekuambia ukweli hata kama ukweli unauma kidogo.
ChatGPT default haiwezi kufanya hivyo. Lakini unaweza kuibadilisha.
Nilichobadili
Kuna siku moja niliiuliza ChatGPT ikague plan niliyokuwa nayo kwa mteja. Plan yenyewe ilikuwa na tundu kubwa katikati, pricing yake haikulingana na value promisely. Mimi nikajua. Lakini nilitaka ku-confirm.
ChatGPT ikanikubalia kila kitu. Ikanipa "5 ways to make this even stronger." Hakuna mahali iliposema "pricing yako haifai kwa offer hii."
Ndipo nikagundua. Sio tatizo la model. Ni tatizo la mazingira. Ninampelekea ChatGPT maswali bila kumwambia nataka anisemee ukweli. Yeye default ni kupendezwa na kila kitu. Nikitaka kitu kingine, lazima niseme.
Basi nikaanza kutumia prompt inayomweleza wazi kabisa aongee nami kama colleague, sio kama fan club. Niliipata, nikaibadilisha mara nyingi hadi ikakaa vizuri. Iko hivi:
Act as a sharp, honest professional colleague, not a helpful chatbot. Treat me as an intelligent adult.
HONESTY
- Be diplomatically honest, not dishonestly diplomatic. If an idea is weak, say so and explain why.
- Vague or hedged answers to avoid friction are a failure. If you have a view, state it.
- Disagree when you disagree. Name flaws in my reasoning before offering alternatives. Do not cave without a real reason.
- Say "I don't know" when you don't. Do not fabricate sources, stats, or features.
- Never open with flattery. No "Great question," "Excellent point," "I love this," or any variant. Start with substance.
- Do not validate my premise by default. If I ask "is my plan good?", assess whether it actually is.
SHAPE
- Answer what I asked. No unrequested sections or tangents.
- Default to the shortest response that fully answers. Long is not thorough.
- Match my expertise level. Skip fundamentals I did not ask about.
- Prose for thinking. Bullets only for parallel items.
- No emojis unless I use them first.
- No closers like "Hope this helps!" End when the answer ends.
UNCERTAINTY
Give your best assessment, labelled as such. State what would change it. Flag what I should verify. Do not hide behind "it depends."
SELF-CHECK BEFORE SENDING
Opened with flattery? Cut it. Hedged? Commit. Added unrequested sections? Delete. Agreed with a flawed premise? Rewrite. Shortest version that answers? If not, cut.
Optimise for my actual outcomes, not my comfort in the moment.
Copy hii yote. Paste kwenye ChatGPT mwanzoni mwa conversation yako mpya. Kisha anza kuuliza maswali yako ya biashara. Au iweke kwenye personalization section ya settings za chatgpt.
Kinachobadilika
Utaona tofauti haraka sana.
Ulikuwa ukipata majibu ya jumla jumla kama "your plan has potential, consider the following factors." Sasa utapata majibu kama "hii sehemu ya plan yako haijulikani. Una-assume wateja watalipa bei hii lakini hujaonyesha sababu. Hapa ndipo inavunjika."
Ulikuwa ukipata "great question!" kila mara. Sasa utapata jibu moja kwa moja.
Ulikuwa ukipata frameworks ndefu ambazo hujauliza. Sasa utapata jibu la swali ulilouliza, basi.
Kwa mara ya kwanza, ChatGPT inaanza kukusaidia kufikiri, badala ya kukukubalia tu.
Jinsi ya Kutumia Hii Vizuri
Prompt yenyewe sio suluhisho. Ni mazingira. Inaseti jinsi ChatGPT itakavyoongea nawe. Lakini wewe bado unabeba kazi ya kuuliza maswali mazuri.
Mifano ya maswali yanayofanya kazi nzuri ukishaweka prompt hii:
"Hii hapa ni plan yangu ya marketing kwa mwezi ujao. Iangalie na uniambie wapi itakwama."
"Nimepanga kuuza huduma yangu kwa bei hii. Nielezee kwa nini inaweza kushindikana."
"Hii caption niliyoandika, ina weakness gani? Sipendi praise. Nataka critique."
"Nafikiria kubadili offer yangu kutoka X hadi Y. Challenge this decision."
Tofauti ya maswali haya na ya kawaida ni kwamba wewe mwenyewe unaingiza expectation yako. Hutaki kukubaliwa. Unataka kufikiri.
Na hiyo ndiyo tofauti kati ya kutumia AI kama toy, na kutumia AI kama mpartner wa biashara.
Tahadhari Moja
ChatGPT bado itafanya makosa. Itakuwa wrong mara nyingine. Prompt hii hairekebishi hilo.
Inachofanya ni kuondoa tabia ya kukubaliana nawe hata pale unapokosea. Bado unabaki na jukumu la kuthibitisha taarifa muhimu, hasa kuhusu takwimu na statistics.
Lakini sasa una colleague anayeweza kukupinga angalau, badala ya shabiki tu ambaye anakukubalia kila kitu.
Hatua Inayofuata
Prompt ni mwanzo tu. Kutumia AI kama business system kabisa kunahitaji zaidi ya prompt moja nzuri. Kunahitaji kujua jinsi ya kuweka context, jinsi ya ku-structure conversations ndefu, jinsi ya kuifanya AI ifanye kazi ndani ya flow ya biashara yako, sio kama kifaa tu cha pembeni.
Hii ndiyo aina ya kazi tunayofanya ndani ya Zillim Growth Club. Sio ma-listicle ya "10 ChatGPT prompts za kila Mjasi." Ni mfumo halisi wa kutumia AI kama infrastructure ya biashara yako.
Kama uko tayari kupeleka hii mbali zaidi, karibu ndani:
Tutaonana huko.
McBenvics
Reply