- Elius' Letters
- Posts
- Umelala? Nimegundua wanaouza online kumbe wanafanya hivi (ni simple)
Umelala? Nimegundua wanaouza online kumbe wanafanya hivi (ni simple)
Elius Letters D001 — Consistency bila strategy ni shughuli, si mauzo
054. Kwanini Kupost Kila Siku Hakukuletei Wateja (Na Nini Kinakuletea Kwa Kweli)
Kuna mtu anaweza kuamka asubuhi, kupiga picha ya bidhaa, kuweka caption, kupost Instagram, kupost TikTok, kisha WhatsApp status — na jioni akasema: "Chief, kwanini napost sana lakini sipati mteja hata mmoja?"
Na ukiangalia kwa juu unaweza kudhani tatizo ni ukosefu wa consistency. Unadhani ungepost zaidi, ungepata wateja zaidi. Lakini ukiangalia kwa ndani, tatizo ni tofauti kabisa: unafanya shughuli nyingi online, lakini huna mfumo unaofanya kila post iwe na kazi maalum kwenye biashara yako.
Hii ndiyo tofauti kati ya mtu anayepost na mtu anayejenga business.
Consistency Bila Strategy Ni Shughuli, Sio Mauzo
Consistency ni nzuri. Lakini consistency peke yake haileti pesa.
Unaweza kuwa mtu wa kupost kila siku, ukapata likes, ukapata comments, ukapata followers na bado ukaendelea kuulizwa "hyo bei gani?" kisha hakuna mtu anayelipa. Hiyo inamaanisha nini? Inamaanisha content yako inafanya kazi moja tu: kuonekana. Haifanyi kazi ya kuwabadilisha watu wanaokuona kuwa wateja.
Biashara haikui kwa kuonekana tu. Inakua pale ambapo mtu anakutazama, anaelewa unamsaidia nini, anaamini unaweza kumsaidia, halafu anaona njia rahisi ya kufanya hatua inayofuata kuuliza, kujisajili, au kulipa.
Kama kila siku unajiuliza "leo nipost nini?" bila kujiuliza "post hii inafanya kazi gani kwa biashara yangu?" basi unajenga shughuli, sio mauzo.
Assignment ya wiki hii: Fungua profile yako ya Instagram au TikTok. Angalia posts 10 za mwisho. Kwa kila moja andika sentensi moja: "Post hii ilikuwa Inafundisha? Ilikwa ni STORY ya kujenga trust?, au ilikuwa inaSELL?" Kama zote zinaonekana za kuSELL au zote zinaonekana random, hapo ndipo tatizo linaanza.
Kila Post Inahitaji Kazi Nne, Sio Kazi Moja
Content yako inapaswa kufanya kazi nne kwa wiki nzima, sio kila post kwa pamoja.
Kuvuta attention — mtu asimame kusoma
Kujenga trust — mtu aamini unajua unachosema
Kuunda desire — mtu aone matokeo ya kufanya kazi na wewe
Kumsogeza kwenye action — DM, WhatsApp, booking, au malipo
Sasa, hapa ndipo watu wengi wanachanganyikiwa. Wanaona content za quotes zinapata likes, wanaona picha za bidhaa zinapata views, wanaona trend inapata comments halafu wanadhani "content zinafanya kazi." Lakini likes si mauzo sasa. Views si malipo mtandaoni. Comments za "bei?" zisizofunga mauzo sio za kufuatilia.
Kama wiki yako yote content unazopoet ni product photos, quotes, na trends bila selling angle, utabaki visible ndiyo lakini unpaid. Na ndiyo maana mtu anaweza kupost kila siku na bado akaishi kwa stress ya mauzo.
Nakupa assignment sasa:
Assignment ya wiki hii: Andika mpango wa posts 4 tu kwa wiki ijayo. Post 1: Ikupe attention. Post 2: Ikupe trust. Post 3: Ujenge desire. Post 4: Usukume mteja kutake action. Usijaribu kufanya kazi nne zote kwenye post moja, gawanya. Mfumo huu ndio unaanza kuondoa kujiuliza "leo nipost nini?"
TEACH·STORY·SELL — Mfumo Unaokomesha Mood Posting
Nataka uelewe kitu muhimu sana.
Usipost kwa mood. Sio kwamba leo unajisikia kupost hiki, kesho haupost, baada ya wiki algorithm inakusahau, engagement inashuka, na business yako inapata baridi.
Mfumo wa TEACH·STORY·SELL unakupa ratio muhimu:
TEACH — fundisha imani au concept moja (kwa nini watu wanapenda aina flan ya bidhaa yako, jibu maswali mteja anayojiuliza kichwani, n.k.)
STORY — onyesha proof: wewe, mteja, au moment halisi
SELL — peleka mtu kwenye hatua ya kununua au kuuliza kwa uzito
Mpangilio wa wiki unaweza kuwa simple: Jumatatu TEACH, Jumanne STORY, Jumatano SELL, Alhamisi TEACH, Ijumaa STORY, Jumamosi SELL, Jumapili TEACH. Ratio hiyo haibadiliki inabadilika tu uzito wa SELL kulingana na jinsi audience yako imejifunza nawe.
Hii ndiyo tofauti kati ya content strategy na content mood. Strategy inakuruhusu kupost hata siku ambayo hujiskii, kwa sababu tayari unajua kazi ya post hiyo. AI inaweza kukusaidia hapa sana, sio kukupa captions rahisi tu, bali kukutengenezea calendar ya wiki nzima kutoka kwenye business profile yako halisi.
Assignment ya wiki hii: Chukua dakika 20. Andika mada 3 za TEACH unazoweza kurudia kila wiki (mfano kama una kampuni ya Usafi: "kwa nini views nyingi hazilipi", "kwa nini DMs zinakufa", "kwa nini offer yako haieleweki"). Hizi ndizo zitakazoondoa blank page kila Jumatatu.
Bila Mfumo, Kupost Zaidi Kunakuongezea Kelele Tu
Tuongee ukweli kidogo ndugu yangu.
Kama huna positioning — watu hawajui unatofautianaje na washindani wako.
Kama huna content system — unapost kwa mood.
Kama huna conversion flow — DMs zinakufa pale wateja wanapoulizia "hyo shngapi boss?"
Kama huna retention — unapata mteja, unampoteza, kisha unalazimika kujitangaza upya kila siku.
Utajikuta unakuwa kama mtu anayepopost zaidi na bado asione mabadiliko. Anaongeza bidhaa, anaongeza trends na kufuata vitu vipya, anaongeza consistency lakini mapengo hayo manne hayajazwi. Na hata ukiongeza bajeti ya matangazo, followers, au idadi ya posts, bado hauuzi zaidi kwa sababu unakuongeza kelele juu ya msingi ambao bado una mashimo.
Mauzo yanatokana na mfumo. Mfumo simple. Mfumo unaoweza kuendeshwa ndani ya dakika 30 kwa siku pale ambapo tayari unaelewa unauza nini, kwa nani, na kwa nini mtu akusikilize wewe.
Sijui umenipata? Japo kuwa wanafunzi wangu wananiita Professor, lakini hii siyo lecture ya kukufanya uache kupost. Ni correction ya kukufanya uache kupost bila kazi.
Posting Ni Sehemu ya Mfumo, Si Mfumo Wenyewe
Lesson ya leo ni simple.
Usidhani tatizo ni ukosefu wa posts nyingi kwenye page. Tatizo ni ukosefu wa mpangilio unaofanya kila post iwe na kazi.
Consistency bila strategy inazalisha shughuli, si mauzo.. hapa ukubali usikatae.
Kila wiki inahitaji mchanganyiko wa content zitakazoleta attention, trust, desire, na action (sell) kwenye biashara yako, sio kimoja tu.
TEACH·STORY·SELL ni strategy inayokomesha mood posting na inakupa calendar inayoendelea hata ukiwa busy.
Kupost zaidi bila kuziba mapengo ya positioning, content, conversion, na retention ni kuongeza kelele tu.
Unaweza Kudhani huwa napoteza muda kukutumia hizi Barua, kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi. Andika mpango wa wiki moja ukitumia hii mbinu ya TEACH·STORY·SELL. Ni rahisi kuliko unavyofikiria lakini sio rahisi kama unaendelea kupost bila kujiuliza kazi ya kila post.
Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim Growth Club)
Kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kuacha kubahatisha online na kuanza kujenga mfumo wako wa kuuza jiunge kwenye Tumia AI Kuuza Online Masterclass.
Ndani ya hili darasa utaondoka ukiwa na business profile yako, calendar ya TEACH·STORY·SELL, na mfumo wa WhatsApp unaobadilisha watu wanaokutafuta kuwa wateja — unaweza kuendesha ndani ya dakika 30 kwa siku.
Uwe na wakati mwema Mjasi.
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply