- Elius' Letters
- Posts
- 184. AI Inaweza Kuongeza Kasi ya Biashara Yako—Au Kuongeza Hatari Zake
184. AI Inaweza Kuongeza Kasi ya Biashara Yako—Au Kuongeza Hatari Zake
Inaweza kukupa majibu kamili, data, majina, references au maelezo ambayo yanaonekana kuwa na maana. Kama hujui vizuri eneo unaloulizia, unaweza ukaamini kwamba umepewa jibu sahihi.
184. AI Inaweza Kuongeza Kasi ya Biashara Yako—Au Kuongeza Hatari Zake
Mfanyabiashara mmoja anaweza kuamka asubuhi, akafungua laptop, halafu ndani ya dakika chache AI ikamsaidia kuandika proposal, kuchambua taarifa za wateja, kujibu email na kupanga kazi za timu.
Inaonekana kama ndoto.
Lakini kuna swali moja ambalo watu wengi hawajiulizi:
AI hiyo ikikosea, nani atabeba gharama?
Kwa sababu kadri tunavyoipa AI kazi nyingi zaidi, ndivyo tunavyoipa access kubwa zaidi kwenye taarifa, mifumo na maamuzi ya biashara yetu. Tatizo sio kwamba AI ni mbaya. Tatizo ni kutumia AI yenye uwezo mkubwa bila kuweka mipaka ya namna inavyopaswa kufanya kazi.
Watu wengi wanaangukia pande mbili.
Wengine wanapuuza kabisa risks za AI. Wanaweka taarifa za wateja, passwords, documents za kampuni na data nyingine muhimu ndani ya AI bila kufikiria mara mbili.
Wengine wanaiogopa AI kiasi kwamba hawaipi nafasi ya kufanya kazi yoyote ya maana.
Njia zote mbili zinaweza kukugharimu.
Jibu sio kuikimbia AI. Jibu ni kuelewa risks zake, halafu kujenga controls zinazokuwezesha kuitumia kwa usalama.
AI Ikikosa Msingi, Inaanza Kutunga
Risk ya kwanza ni hallucination.
Hallucination ni pale AI inapokupa taarifa inayoonekana kuwa sahihi, imeandikwa vizuri na ina confidence, lakini taarifa yenyewe sio ya kweli.
Hili ndilo linalofanya hallucination iwe hatari.
Mara nyingi AI haisemi, “Sina uhakika.”
Inaweza kukupa majibu kamili, data, majina, references au maelezo ambayo yanaonekana kuwa na maana. Kama hujui vizuri eneo unaloulizia, unaweza ukaamini kwamba umepewa jibu sahihi.
Kadri models zinavyokuwa bora, kiwango cha hallucination kinaendelea kupungua. AI za sasa zina uwezo mkubwa zaidi ukilinganisha na models za miaka michache iliyopita.
Lakini risk haijaondoka.
AI inaweza kuchanganyikiwa inapopewa maelekezo mengi, documents nyingi au context isiyopangwa vizuri. Inaweza kuunganisha taarifa ambazo hazihusiani, kujaza sehemu ambazo hazina data au kutoa hitimisho ambalo halijatokana na ushahidi uliopo.
Control yake kubwa ni grounding.
Grounding ni kuhakikisha AI ina taarifa zote muhimu inazohitaji kufanya kazi, na inaelekezwa kutumia taarifa hizo badala ya kubuni majibu kutoka kwenye hewa.
Kama unataka AI iandike proposal ya kampuni yako, usiishie kusema:
“Niandikie proposal nzuri.”
Mpe bei zako, huduma zako, aina ya wateja unaowahudumia, ushahidi wa kazi zilizopita, masharti yako na mfano wa proposal unayotumia.
Unapompa msingi mzuri, unapunguza nafasi ya AI kutunga.
Lakini kumbuka: hata AI iliyokuwa grounded inahitaji ukaguzi wa binadamu kabla ya taarifa muhimu kutumwa kwa mteja, kutumika kufanya maamuzi au kuchapishwa hadharani.
Data Yako Sio Chakula cha Kila AI
Risk ya pili ni data exposure.
Watu wengi wanazungumza na AI kama wanavyozungumza na rafiki yao wa karibu. Wanapaste mikataba, majina ya wateja, taarifa za kifedha, health records, passwords, API keys na documents za ndani za kampuni.
Lakini data nyingine hazipaswi kuwekwa kwenye mfumo wowote bila kufikiria jinsi zitakavyohifadhiwa, nani anaweza kuzifikia na masharti gani yanatumika.
Hili ni muhimu zaidi kwenye maeneo yenye taarifa nyeti kama afya, sheria, fedha, serikali na taasisi zinazohifadhi taarifa binafsi za watu.
Kabla hujaweka data ndani ya AI, jiulize:
Je, AI inahitaji kweli taarifa hii ili kufanya kazi?
Naweza kuondoa jina, namba ya simu au taarifa inayomtambulisha mteja?
Ni nani mwenye access ya account, workspace au conversation hii?
Data hii ikionekana na mtu mwingine, inaweza kuleta madhara gani?
Sera za kampuni yetu zinaruhusu data hii kutumiwa kwenye mfumo huu?
Kanuni rahisi ni hii: usimpe AI data nyingi kuliko anazohitaji.
Kama unataka AI ichambue complaints za wateja, mara nyingi haitaji majina yao, namba zao za simu au taarifa zao za malipo. Inaweza kufanya kazi kwa kutumia complaints zilizofichwa identity.
Control nyingine ni permissions.
AI agent akipewa access ya Google Drive, Gmail, database au mfumo mwingine, usimpe uwezo wa kufanya kila kitu kwa sababu tu uwezo huo upo.
Kama anahitaji kusoma document, mpe read-only access.
Kama anahitaji kuandaa email, anaweza kuruhusiwa kutengeneza draft bila kuruhusiwa kuituma.
Kama anahitaji kuchambua taarifa, usimpe ruhusa ya kufuta au kubadilisha data.
AI haipaswi kupewa funguo za jengo zima wakati kazi yake ni kufungua chumba kimoja.
AI Ina Bias, Access na Maslahi ya Mfumo Iliotengenezwa Ndani Yake
Risk ya tatu ni kuamini AI kama hakimu asiye na upande.
AI models zimefundishwa kwa data tofauti, zimejengwa na kampuni tofauti na zina sheria tofauti kuhusu majibu yanayoruhusiwa. Kwa hiyo, models mbili zinaweza kupewa swali lilelile na kutoa majibu tofauti.
Hii inaonekana sana kwenye masuala ya imani, siasa, mahusiano, maadili, utamaduni na ideologies.
Hata kwenye biashara, AI inaweza kupendelea njia moja ya kufanya mambo kwa sababu ndio njia iliyoonekana sana kwenye training data yake, si kwa sababu ndio njia bora kwa mazingira yako.
Kwa hiyo, usichukulie kila jibu la AI kama fact.
Kwa mambo yanayohusisha judgement, linganisha models tofauti, tafuta sources na uangalie kama jibu linakubaliana na mazingira yako.
Risk nyingine inayokua ni unauthorized access.
Tunapoipa AI uwezo wa kutumia tools, kufungua files, kuendesha commands au kuunganisha mifumo, inaweza kujaribu kufanya kitendo ambacho hakikupangwa vizuri kwenye instructions.
Hii ndiyo sababu AI agent mwenye uwezo wa kufanya kazi lazima awe na mipaka.
Control nzuri ni human approval.
Kabla AI haijafanya kitendo chenye athari kubwa, inapaswa kurudi kwa binadamu kuomba ruhusa.
Kwa mfano:
AI anaweza kuandaa invoice, lakini binadamu athibitishe kabla haijatumwa.
AI anaweza kutambua leads wa kufuatilia, lakini asitume ujumbe kwa mamia ya watu bila approval.
AI anaweza kuandika mabadiliko kwenye mfumo, lakini asiyapeleke live bila ukaguzi.
AI anaweza kupendekeza kufuta taarifa, lakini asiwe na uwezo wa kuzifuta moja kwa moja.
Hii haimaanishi binadamu lazima afanye kila kazi. Maana yake ni binadamu anabaki na control kwenye maamuzi yenye risk kubwa.
Biashara Yako Isifungwe na Model Moja
Risk ya nne ni vendor dependence.
Unaweza kujenga mfumo mzima wa biashara juu ya model moja, kampuni moja au platform moja. Baada ya muda, workflows zako, prompts zako na processes zako zote zinaanza kuitegemea.
Halafu kampuni hiyo ikibadilisha bei, rules, limits au features, biashara yako inaanza kutikisika.
Haimaanishi usitumie ChatGPT, Claude, Grok, Gemini au model nyingine. Maana yake ni usijenge biashara yako kwa namna ambayo model moja ikipotea, kampuni nzima inasimama.
Jenga process inayoweza kuhamishwa.
Data zako muhimu zihifadhiwe kwenye mifumo unayo-control. Instructions za AI ziandikwe vizuri. Procedures zako zisiwe zimefungwa ndani ya chat moja. Na inapowezekana, uwe na fallback.
Fallback ni mpango wa AI kufanya nini pale inaposhindwa.
Kama model moja haiwezi kumaliza kazi, mfumo unaweza kuhamisha kazi kwenda kwenye model nyingine. Kama AI hana uhakika, anaweza kuacha kazi na kuomba msaada wa binadamu. Kama integration imekataa, taarifa inaweza kuhifadhiwa kwenye queue badala ya kupotea.
Lakini kuwa na fallback pekee haitoshi.
Unahitaji logging.
Logging ni kurekodi AI amefanya nini, ametumia taarifa gani na matokeo gani yametolewa. Hii inakusaidia kurudi nyuma na kuelewa kilichotokea pale kuna kosa.
Hapo ndipo tunakutana na risk nyingine: lack of auditability.
AI inaweza kukupa jibu, lakini isiwe rahisi kuelewa kila hatua iliyofikisha kwenye jibu hilo. Ndiyo maana kwenye kazi muhimu, huwezi kutegemea jibu la mwisho pekee.
Unahitaji source, logs, history ya actions na approvals zilizotolewa.
Kama huwezi kujua mfumo wako umefanya nini, ni vigumu kuuboresha. Na ukitokea umefanya kosa, ni vigumu kujua sehemu ya kurekebisha.
Mfumo Salama Haujengwi Mara Moja
Baada ya kuweka grounding, permissions, approvals na logs, bado unatakiwa kufanya testing.
Usisubiri AI afanye kosa mbele ya mteja ndio ugundue mfumo wako una tatizo.
Mpe majaribio magumu.
Jaribu kumpa instructions zinazokinzana. Jaribu kuona kama anaweza kufikia document asiyoruhusiwa. Angalia anafanya nini akikosa taarifa. Test kama anajua kusimama na kuomba msaada badala ya kubuni jibu.
Halafu jenga incident response.
Incident response ni process ya kufuata pale AI inapofanya kosa au kuleta risk.
Mfumo wako unaweza kueleza:
Nani anatakiwa kuarifiwa?
Access ipi inapaswa kuzimwa?
Data gani inapaswa kukaguliwa?
Mteja anahitaji kupewa taarifa?
Ni instruction, permission au process gani inapaswa kurekebishwa?
Biashara kubwa hazijengwi kwa kuamini kwamba makosa hayatokei. Zinajengwa kwa kujua jinsi ya kuyagundua mapema na kuyashughulikia kabla hayajawa makubwa.
Hii ndiyo tofauti kati ya kutumia AI kama chatbot na kutumia AI kama operator.
Chatbot unamuuliza swali na unachukua jibu.
Operator ana context, mipaka, procedures, permissions, memory, logs na hatua za kufuata anapokwama.
Kama wewe unatumia AI kila siku lakini kila session inaanza upya, taarifa zako zimetawanyika na AI hana rules za namna ya kufanya kazi, kuna nafasi kubwa hujajenga operator bado.
Kama unataka kuelewa namna ya kujenga mfumo huo kwa vitendo, tulitengeneza AI Operator Masterclass (operator.zillim.digital) kwa ajili ya founders, consultants na builders wanaotaka AI ifanye kazi ndani ya mfumo badala ya kutegemea prompts za siku moja.
AI Yenye Nguvu Bila Mipaka Ni Risk, Sio Mfumo
Ground AI yako kwa data sahihi ili isipike majibu inapokosa taarifa.
Linda data za wateja na kampuni kwa kumpa AI taarifa anazohitaji tu.
Tumia permissions na human approval kuzuia AI kufanya actions zenye athari bila ruhusa.
Weka logs, testing, fallback na incident response ili uweze kuona, kurekebisha na kujifunza kutokana na makosa.
Usijenge biashara inayokufa model moja au vendor mmoja akibadilika.
Lengo sio kuondoa risk zote. Hilo haliwezekani kwenye AI, wala kwenye biashara yoyote.
Lengo ni kujua risk zako ziko wapi, kuzipunguza na kuhakikisha binadamu bado ana control ya maamuzi muhimu.
AI inaweza kukusaidia kukua kwa kasi, kuhudumia wateja wengi na kupunguza kazi zinazojirudia. Lakini speed bila control inaweza kukupeleka sehemu usiyotaka kwa haraka zaidi.
Jifunze kutumia AI, lakini usiishie kujifunza prompts.
Jifunze kujenga mfumo.
Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim)
Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi.
Na kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni — jiunge kwenye community yetu kupata AI For Social Media Marketing Training:
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply