- Elius' Letters
- Posts
- 188. Jinsi ya Kuuza Dar Ukiwa Arusha
188. Jinsi ya Kuuza Dar Ukiwa Arusha
Mteja hasemi “basi” kwa sababu ya umbali. Anasema hivyo kwa sababu haamini mzigo utafika.
188. Jinsi ya Kuuza Dar Ukiwa Arusha
Mteja hasemi “basi” kwa sababu ya umbali. Anasema hivyo kwa sababu haamini mzigo utafika.
Dada mmoja alikuwa dukani. Mteja wa Dar anachagua, anaomba picha, anasema nitakuja nitachukua. Halafu anageuza: nifungie delivery Kigamboni.
Dada anasema sina uwezo Kigamboni, lakini naweza kutuma. Utapokea kesho asubuhi.
Mteja: “Hee. Basi. Basi.”
Na anatoweka.
Hiyo ndiyo moment nyingi ya Mjasi mkoani unaiona, unaiita tatizo la delivery. Au tatizo la wateja wa Dar kuwa “wakali.” Au tatizo la Arusha, Mwanza, Dodoma, Moshi.
Sio.
Bidhaa inaweza kuwa nzuri. Bei inaweza kuwa sawa. Picha zinaweza kuwa safi. Lakini mara tu mteja anaposikia uko mkoani, kichwani mwake swali linabadilika. Si “napenda hii?” Tena ni “nikituma pesa, nitapata mzigo kweli? Ukishapokea hela, utanijibu? Na nikitapeliwa, nitafanya nini?”
Unauza bidhaa. Yeye ananunua imani. Imani ikishuka, oda inakufa kabla hujawahi kusema bei.
Pengo la Imani
Watu wanafikiri marketing ni kuonyesha bidhaa mpaka mtu achoke na kukuona. Kwa mteja wa mkoa mwingine, marketing ni kitu kingine: unamwondolea hofu.
Yuko Dar, wewe Arusha. Hajaona duka lako. Hajashika kitu. Anakuona kwenye Instagram, anapenda, kisha anasoma bio au anakuuliza “uko wapi?” Jibu lako linakuwa kisu.
“Niko Arusha.”
Hapo hapo risk inapanda. Si kwa sababu Arusha ni mbaya. Ni kwa sababu hana ushahidi kwamba watu kama yeye walikuwahi kukuamini, na wakapata walichoahidiwa.
Kama unataka kuuza nje ya mkoa wako, usitumie account yako kama catalogue. Catalogue haisemi “nitafika.” Inasema “tazama tu.”
Jenga ushahidi.
Ushahidi si Wewe
Ushahidi mara nyingi hautoki kwako. Hautoki kwa wewe kuapa “sisi tunatuma, tumaini.” Unatoka kwa mtu mwingine kama yeye.
Mtu wa Mbezi, Kigamboni, Sinza, au Ubungo, akionyesha amepokea mzigo kutoka Arusha, hiyo inafanya kazi kubwa kuliko post kumi za maua, décor, au cosmetics zako.
Hiyo ndiyo UGC. User generated content. Content inayotengenezwa na watumiaji, si na wewe ukiwa studio.
Mfano rahisi: mteja wa Dar anashika kamera. “Mimi napenda décor. Nikakutana na huyu kwenye social media. Yuko Arusha. Nilijiuliza, kweli nitapata mzigo? Nikamwamini, nikamtumia pesa. Leo tuna-unbox pamoja.”
Hiyo si advertisement. Hiyo ni sababu ya kukuamini.
Na ndiyo, asilimia kubwa ya watu wanaotengeneza UGC wanahitaji uwalipe. Lipe. Content hii inafanya kazi ambayo posting bidhaa kila asubuhi haifanyi: inatengeneza imani ili mtu mwingine aamini anunue. Kama ni mteja wako, mpe ofa nzuri. Usitarajie watu wakujengee trust bure, kisha wewe unauza.
Pamoja na UGC, tumia vitu vidogo vinavyoonekana “boring” lakini vinaua shaka: receipts, screenshots za WhatsApp, “nashukuru, nilikuwa sijui kama nitaweza kupokea mzigo kutoka Arusha nikiwa Dar.” Hiyo screenshot moja inaweza kufanya kazi kuliko caption ndefu ya “quality guaranteed.”
Bidhaa Bidhaa Bidhaa si Strategy
Ukiingia kwenye account ya dada huyo, unaona picha za bidhaa. Huduma. Story za kuongea. Lakini hakuna mahusiano ya wazi kati ya hofu ya mteja na kile anachojaribu kuuza.
Mteja anaogopa kutuma pesa mkoani. Account inasema “tazama hii bouquet. Tazama hii. Tazama hii.”
Hakuna content inayojenga authority. Hakuna “hivi ndivyo oda inavyopokelewa, inavyopackiwa, inavyotumwa, inavyofika.” Hakuna mteja wa Dar akifungua mzigo. Kwa hiyo mtu akigundua yupo Arusha, hana kitu cha kushika isipokuwa hatari.
Onesha process yako.
Mteja akiweka oda saa hivi, unaangalia stock. Unamwongezea ofa. Unafunga. Inamfikia ndani ya masaa 24. Akiweka leo, kesho asubuhi yuko na mzigo. Hiyo si “content ya kujivunia.” Hiyo ni content inayouza, kwa sababu inamjibu swali alilokuwa na aibu kuuliza.
Delivery yenyewe ni sehemu ya offer. Kama unaweza kuwa na mawakala au partners kwenye mikoa muhimu, mteja anaenda kuchukua mzigo mwana kwa mwana. Trust inapanda, si kwa sababu umepaza sauti, ni kwa sababu umepunguza umbali wa hatari.
Cash on delivery unaweza kuizungumza. Lakini usiifanye msaada wako mkuu. COD inasema wewe bado haamini, yeye bado haamini, mnaogopana. Ikiwa unaitumia, iwe conditional: deposit, kisha mabaki akipokea. Au escrow: pesa inakaa katikati, mzigo ukifika, unalipwa. Bora zaidi: jenga imani kiasi mtu analipa full.
Usikuwe na kesi hata moja ya mteja aliyewahi kuweka order asipate alichokitaka. Hiyo kesi moja inaua kumi zijazo.
Huwezi Kuomba Watu Wakuamini
Mteja wa Dar hakukataa kwa sababu uko Arusha. Amekataa kwa sababu hakuona sababu ya kukuamini.
Ushahidi unatoka kwa mtu kama yeye, si kwa wewe kuapa.
Account inayoonyesha bidhaa tu inauza catalogue, si imani.
Process, receipts, UGC, na namna ya kufikisha mzigo ni marketing, si extras.
Kama unauza kwenye Instagram na WhatsApp na bado DM inakufa mara tu mtu anaposikia uko mkoani, kuna darasa dogo tulilolijenga kwa hilo hasa, Tumia AI Kuuza Online.
Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi.
Leo chukua account yako. Hesabu post kumi za mwisho. Ngapi ni bidhaa tupu, ngapi zinaonyesha mtu halisi akipokea, akifungua, akishukuru. Kama zote ni bidhaa, huo ndio pengo.
Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim)
Kama wewe ni Mjasi au Content Creator na uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni, jiunge kwenye community yetu kupata AI For Social Media Marketing Training:
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply