- Elius' Letters
- Posts
- 187. Watu Wanaotengeneza Milioni 150 Kwa Mwezi Wamenifundisha Nini?
187. Watu Wanaotengeneza Milioni 150 Kwa Mwezi Wamenifundisha Nini?
Na kadri ninavyoendelea kuwaangalia, nimeanza kuona wazi zaidi kile ninachopaswa kufanya ili kufikia lengo langu mwenyewe: kutengeneza dola 50,000 kwa mwezi ndani ya miaka mitano ijayo.
187. Watu Wanaotengeneza Milioni 150 Kwa Mwezi Wamenifundisha Nini?
Kuna tofauti kubwa kati ya kuambiwa kwamba inawezekana na kukaa karibu na watu wanaokuonyesha kwamba inawezekana.
Baadhi ya partners wangu wanafanya wastani wa zaidi ya milioni 150 kwa mwezi. Wengine wanafika zaidi ya milioni 200 kwa mwezi, huku wakibaki na faida ya milioni 60 hadi 100 baada ya gharama.
Namba hizi zinaweza kusikika kubwa sana. Unaweza kuzisikia na kufikiria labda watu hawa wana bahati, wana connections ambazo wewe huna, au walianza na mtaji mkubwa.
Lakini baada ya kuwaangalia kwa karibu, nimegundua mafanikio yao hayajatokana na kitu kimoja cha ajabu.
Yametokana na mambo machache ambayo wamekubali kuyafanya kwa muda mrefu, bila kuchoka na bila kutegemea hamasa ya siku moja.
Na kadri ninavyoendelea kuwaangalia, nimeanza kuona wazi zaidi kile ninachopaswa kufanya ili kufikia lengo langu mwenyewe: kutengeneza dola 50,000 kwa mwezi ndani ya miaka mitano ijayo.
Sio kwa kutamani namba hiyo kila siku, bali kwa kujenga aina ya biashara inayoweza kuizalisha.
Wamejenga soko kabla ya kuhitaji kuuza
Partners wangu wanatumia social media bila kuchoka.
Wanazungumza na watu. Wanashare wanachofanya. Wanaonyesha bidhaa zao, matokeo ya wateja, safari zao na mambo wanayojifunza. Hawatumii social media pale tu wanapokuwa na kitu cha kuuza.
Wamejenga community inayowajua, inayowaamini na inayofuatilia kazi zao.
Hili limenifundisha kwamba community sio idadi ya followers tu. Ni kundi la watu wanaoelewa unawakilisha nini na wanaamini unaweza kuwasaidia.
Watu wengi tunataka kupata wateja bila kupitia kipindi cha kujenga uaminifu. Tunataka post content moja leo, kisha kesho tupokee orders nyingi. Tukikosa mauzo tunasema social media haifanyi kazi.
Partners wangu wamefanya social media kuwa sehemu ya biashara zao, sio kazi ya pembeni wanayofanya wanapopata muda.
Nikitaka kutengeneza dola 50,000 kwa mwezi, nitahitaji zaidi ya bidhaa nzuri. Nitahitaji soko linalonijua kabla hata sijalizindulia bidhaa inayofuata.
Ndiyo maana nitaendelea kujenga audience na community kwa muda mrefu. Nitaendelea kuzungumza na watu ninaotaka kuwahudumia, kuelewa matatizo yao na kuwa mtu wanayemkumbuka wanapohitaji suluhisho.
Content kwao si tukio kubwa
Kitu kingine nilichogundua ni jinsi wanavyorahisisha content.
Hawasubiri kila video iwe masterpiece. Hawatumii siku nzima kutafuta wazo ambalo halijawahi kuzungumziwa na mtu mwingine duniani.
Wanachukua kile wanachofanya kila siku na kukiweka mbele ya watu.
Swali la mteja linaweza kuwa content. Kosa walilofanya linaweza kuwa somo. Ushindi mdogo unaweza kuwa story. Mchakato wa kutengeneza bidhaa unaweza kuwa video. Maoni yao kuhusu biashara yanaweza kuwa post.
Hii ndiyo sababu wanaweza kutokea mara nyingi bila content kuwachosha.
Ukifanya kila post ionekane kama production ya televisheni, utachoka. Lakini ukitambua kwamba biashara yako tayari inakupa kitu cha kusema kila siku, content inakuwa nyepesi.
Nimeamua kufanya vivyo hivyo.
Sitaki content iwe kitu ninacholazimisha baada ya kazi nyingine kuisha. Nataka iwe njia ya kuandika na kuonyesha safari ninayoishi. Kujenga bidhaa, kuwahudumia wateja, kutumia AI, kufanya makosa, kuboresha mifumo na kukutana na changamoto—haya yote ni sehemu ya story.
Lengo si kuonekana perfect. Lengo ni kuwasaidia watu kuona ninachojenga, ninachoamini na matokeo ninayoweza kuwasaidia kuyafikia.
Wanainvest kabla hawajajisikia tayari
Watu hawa hawaogopi kuwekeza ndani yao.
Wananunua maarifa. Wanaajiri watu wenye uwezo. Wanalipia tools zinazorahisisha kazi. Wanaingia kwenye mazingira yenye watu wanaowasukuma kufikiria kwa ukubwa zaidi.
Watu wengi tunaona kuwekeza kwenye elimu, technology au team kama kupoteza pesa. Tunataka biashara ikue kwanza, ndipo tuanze kuwekeza.
Lakini biashara mara nyingi hukua baada ya wewe kuwekeza, sio kabla.
Kila hatua mpya ya biashara inahitaji version mpya ya mwenye biashara. Kuna skills ambazo huwezi kuendelea kuzikwepa. Kuna watu ambao utahitaji msaada wao. Kuna mifumo ambayo itahitaji fedha kabla haijaanza kurudisha fedha.
Nilichojifunza ni kwamba kuwa makini na pesa hakumaanishi kuogopa kuitumia. Inamaanisha kujua ni matumizi gani yanajenga uwezo wa biashara kuzalisha zaidi kesho.
Katika miaka yangu mitano kuelekea dola 50,000 kwa mwezi, nitahitaji kuwekeza kwenye maarifa, watu, mifumo na relationships. Sitafanya hivyo kwa papara, lakini pia sitaruhusu hofu ya kupoteza pesa inizuie kujenga uwezo wa kutengeneza pesa zaidi.
Mauzo yao yanaungwa mkono na mfumo
Mauzo makubwa yanaonekana vizuri kwenye Instagram, lakini nyuma yake kuna kitu ambacho hakionekani sana: fulfillment.
Partners wangu hawajaishia kuwa wazuri kwenye kuuza. Wana mfumo wa kuhakikisha mteja anapata kile alichoahidiwa.
Kuna watu, majukumu, hatua, ratiba na namna ya kupima kama kazi imefanyika vizuri. Biashara haiishi ndani ya kichwa cha founder peke yake.
Na si fulfillment tu. Biashara nzima inaendeshwa kama mfumo.
Content inaleta attention. Community inajenga trust. Offer inabadilisha attention kuwa mauzo. Fulfillment inampa mteja matokeo. Matokeo yanazalisha ushahidi na referrals. Kisha ushahidi huo unarahisisha mauzo yanayofuata.
Hapo biashara inaanza kujilisha yenyewe.
Watu wengi tunataka mapato ya biashara kubwa, lakini bado tunaendesha biashara kwa kukumbuka kila kitu kichwani. Kila order inategemea sisi. Kila mteja anahitaji sisi. Tukipumzika, biashara nayo inapumzika.
Hiyo inaweza kutengeneza kipato, lakini ni vigumu kutengeneza dola 50,000 kwa mwezi kwa miaka mingi kupitia juhudi za mtu mmoja.
Ndio maana sitajenga mauzo pekee. Nitajenga mashine ya mauzo na fulfillment inayoweza kurudia matokeo bila kutegemea nguvu zangu kila saa.
Dola 50,000 kwa mwezi itajengwa kabla haijafika
Namba hiyo ni takribani milioni 130 za Kitanzania kwa mwezi, kutegemea exchange rate. Leo inaweza kuonekana mbali, lakini sasa nimekaa karibu na watu wanaofanya kiasi hicho na zaidi.
Wamenisaidia kuona kwamba lengo hilo halihitaji miujiza. Linahitaji tabia, uwezo na mifumo inayolingana nalo.
Nitatumia social media kwa consistency na kujenga community inayoniamini.
Nitarahisisha content ili niweze kuonekana na kufundisha bila kuchoka.
Nitawekeza ndani yangu, kwenye watu sahihi na kwenye tools zinazoongeza uwezo wetu.
Nitajenga fulfillment inayowapa wateja matokeo bila kila kitu kunitegemea mimi.
Nitaendesha biashara kama mfumo unaoweza kupimwa, kuboreshwa na kukua.
Miaka mitano si muda wa kusubiri kuona kama lengo litatimia. Ni muda wa kuwa mtu anayeweza kulibeba.
Kila post, kila skill mpya, kila mteja ninayemsaidia na kila mfumo ninaoujenga ni kura ninayoipiga kwa maisha ninayotaka. Nikirudia mambo haya kwa muda wa kutosha, dola 50,000 kwa mwezi haitakuwa tena ndoto niliyoandika. Itakuwa matokeo ya biashara niliyojenga kwa makusudi.
Jifunze Kujitangaza Online na AI
Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Chagua jambo moja kati ya haya matano na anza kulifanyia kazi wiki hii.
Na kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni, jiunge kwenye community yetu kupata AI For Social Media Marketing Training:
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply