187. Jinsi ya Kuuza Bila Kupigiana Simu na Wateja

Kama hutaki kufanya kitu fulani kwenye biashara yako, inabidi utumie mechanism nyingine, mbinu nyingine, au strategy nyingine ambayo inaleta matokeo yale yale bila wewe kufanya kile kitu ambacho hupendi kufanya.

187. Jinsi ya Kuuza Bila Kupigiana Simu na Wateja

Na leo nataka nikufundishe jinsi ya kuuza bila kuongea na watu kwenye simu.

Kama wewe sio mpenzi kabisa wa kupiga simu, basi hili darasa ni lako.

Mimi binafsi sipendi sana kuonana na watu. Lakini pia sipendi kupigiana simu na watu kwa sababu sometimes nakuwa kwenye vikao na watu wengine, nipo nafanya kitu kingine, au simply sitaki simu ikatishe kile ninachofanya.

Nikiwa hapa ninafundisha halafu mtu ananipigia simu, yani hasira kidogo zinanipanda.

Lakini bado naweza kuuza.

Kwa sababu nimejifunza kitu kimoja.

Kama hutaki kufanya kitu fulani kwenye biashara yako, inabidi utumie mechanism nyingine, mbinu nyingine, au strategy nyingine ambayo inaleta matokeo yale yale bila wewe kufanya kile kitu ambacho hupendi kufanya.

Na kwenye mauzo, kuna namna unaweza kupunguza sana kupigiana simu na wateja wako.

Acha content zianze mazungumzo

Kitu cha kwanza, tumia content.

Lakini usitumie content kufanya sales tu.

Acha content zianze conversation.

Hapa ndipo wafanyabiashara wengi wanapokosea.

Unatengeneza tangazo ambalo kazi yake ni kuonesha bidhaa yako tu.

Tuseme unauza magari.

Umepiga picha ya gari. Umeonesha lina CC ngapi, mileage kiasi gani, mwaka gani na bei yake.

Basi.

Lakini hujaanzisha mazungumzo yoyote.

Matokeo yake mteja akiona gari lazima akupigie simu kuuliza maswali ambayo ungeweza kuyajibu kabla hajakupigia.

“Bei gani?”

“Kuna rangi nyingine?”

“Mnafanya financing?”

“Mnafanya delivery?”

Badala ya kuonesha bidhaa tu kama watu walivyokuwa wanafanya zamani, anza kupiga story na wateja wako kupitia content zako.

Waeleze kwa nini mtu anaweza kupenda hilo gari.

Waeleze kwa nini mtu mwingine hatalipenda.

Ongelea maswali ambayo kawaida wanakuuliza.

Ongelea hofu zao.

Hayo ndiyo mazungumzo.

Kwa sababu unaweza kujikuta umemalizana na mteja wako kwenye content, comments au DM kabla hata hajataka kukupigia simu.

Content zako zikifanya kazi vizuri, mteja anakuja akiwa tayari amekuelewa na ameanza kukuamini.

Mnaweza kuchat mpaka akanunua.

Hicho ndicho kitu ambacho mimi nakipenda.

Nataka biashara yangu iweze kuwauzia wateja wangu bila wateja kulazimika kuongea na mimi, bila kunipigia simu, na bila kulazimika kuonana na mimi ana kwa ana.

Kwa sababu huduma zangu watazipata hivyo hivyo.

Mtoe kwenye content, mpeleke WhatsApp

Sasa nataka ufikirie kitu kimoja.

Tuseme tayari umetengeneza content na mtu ameonesha interest.

Usimwambie akupigie simu.

Mpeleke WhatsApp.

Kwa sababu WhatsApp ni sehemu ya chat. Ni sehemu ya voice notes. Ni sehemu ambayo unaweza kumjibu mteja kwa muda ambao wewe upo available.

Na kama wewe ni mfanyabiashara ambaye uko busy sana, hii ni muhimu zaidi.

Unaweza kuwa unatembea. Una meeting. Unaongea na high-level customers. Unafanya kitu kingine.

Huna muda wa kila mtu kukupigia simu akuelezee shida zake kwa dakika 20.

WhatsApp inakupa control ya muda wako.

Lakini kuna kitu kingine muhimu zaidi.

Mteja anapotumia messages, unapata reference.

Zile chats zako na mteja wako, zile data ambazo mteja wako anakupatia, zinaweza kukusaidia kumuelewa zaidi baadaye.

Ukianza kuongeza mifumo ya kutunza wateja wako — tunaita Customer Relationship Management System — unaweza kuhifadhi mahusiano yako na wateja vizuri zaidi.

Kwenye simu, mteja akikuambia kila kitu, kichwa chako ndiyo kinatakiwa kitunze kumbukumbu zote.

Lakini kwenye WhatsApp, conversation ipo.

Kwa hiyo badala ya kulazimika kuzungumza na kila mteja, fanya content zako zianzishe mazungumzo, halafu mtoe mteja kwenye content na umpeleke WhatsApp au DM.

Badala ya kuwa muuzaji, kuwa daktari

Hili ni muhimu sana.

Mteja akikutafuta, usianze kumshawishi.

Mdiagnose.

Badala ya kuwa muuzaji, kuwa daktari.

Muulize anahitaji nini.

Muulize ana shida gani ambayo anadhani bidhaa yako inaweza kumsaidia.

Muulize kwa nini anachagua hiyo bidhaa.

Muulize anataka kupata matokeo gani.

Hiyo ndiyo diagnosis.

Lakini hii kitu huwezi kuifanya shambashamba. Ovyo ovyo.

Lazima uwe na structured conversations.

Mteja akiulizia bei, unajua cha kusema.

Mteja akisema kitu fulani, unajua swali gani linafuata.

Mteja akiwa na objection fulani, unajua jinsi ya kuendelea na conversation.

Kwa sababu lengo sio kumlazimisha anunue.

Lengo ni kuelewa shida yake.

Na ukishaelewa shida yake, sasa unaweza kufanya kitu kinachofuata.

Usipitch. Recommend.

Badala ya kumuuzia mteja wako, recommend.

Usianze:

“Jamani nunua hii bidhaa. Kwanza sisi tuna bidhaa hii, itakusaidia hiki na hiki…”

No, no, no.

Umeshafanya diagnosis.

Umeshakuwa daktari.

Umeelewa shida ya mteja wako. Umeelewa kwa nini amekutafuta. Umeelewa ni kitu gani kwenye maisha au biashara yake kinamsumbua ambacho huduma yako inaweza kusaidia.

Sasa mpe recommendation.

Mwambie:

“Kwa changamoto yako, mimi ninachoona kitakachokufaa ni kitu fulani.”

Hapo humpitch.

Unarecommend.

Na kuna tofauti kubwa sana.

Kwa sababu sasa recommendation yako inatokana na conversation mliyokuwa nayo.

Kwa hiyo kuanzia leo wewe ni daktari.

Mtu akikuuliza udaktari umepewa na nani, mwambie McBenvics amenipa.

Lakini uwe daktari kwenye vitu vyako tu. Sio uende hospitali kutibu watu, utaua watu.

Simu itumike pale ambapo ni necessary

Sijasema usipige simu kabisa.

Tumia calls pale ambapo ni necessary.

Unaweza kuzungumza na mteja kwenye chats halafu ukaona kabisa hapa huyu ni serious customer. Ana nia ya kununua, ana budget, lakini kuna kitu kimoja kinahitaji mazungumzo marefu.

Hapo mpigie simu.

Lakini call inakuwa hatua ya mwisho, sio hatua ya kwanza.

Content zako zinatakiwa zimuondolee mteja madukuduku mengi kabla hajaja.

Akifika WhatsApp akiwa bado na madukuduku, mdiagnose kupitia structured conversations.

Ukishagundua changamoto yake inaweza kutatuliwa na bidhaa au huduma zako, mpe recommendation inayomfaa yeye.

Ukiona yote hayo yamefanyika lakini bado huyu mteja anaonesha nia ya kununua na kuna umuhimu wa kuzungumza, hapo unaweza kwenda kwenye simu.

Point yangu ni kupunguza idadi ya simu ambazo unazungumza na wateja unnecessarily.

Mteja anakupigia kuuliza bei?

Huyo mngeweza kumalizana kwenye content toka mwanzo.

Mteja anakupigia kuuliza kama mnafanya delivery?

Hata kama content zako hazijasema, mngeweza kumalizana WhatsApp.

Hakuna sababu ya kupoteza dakika 20 kwenye simu kuelezea kitu ambacho kingeweza kujibiwa kwa message mbili.

Na sasa tunaingia kwenye agentic era ambayo AI inaweza kuwa sehemu ya mfumo huu. Hapa ndipo biashara zinaweza kutumia AI kusaidia kutengeneza content, kupanga responses za WhatsApp, kuhifadhi taarifa za wateja, kufanya follow-up na kusaidia biashara kuuza bila kila conversation kumtegemea mwenye biashara.

Kama unauza kwenye Instagram na WhatsApp na unataka kujenga mfumo kama huu, haya ndiyo mambo tunayojifunza kwenye Tumia AI Kuuza Online Masterclass — jinsi ya kutumia AI kujitofautisha, kutengeneza content, kuuza ndani ya DM na WhatsApp, na kutunza wateja wako. Unaweza kuangalia maelezo kwenye tumia.zillim.digital.

Biashara yako isiwe simu yako

  1. Acha content zianzishe mazungumzo — mteja asije kwako akiwa na maswali yote ambayo ungeweza kuyajibu kabla.

  2. Mtoe kwenye content, mpeleke WhatsApp — hapo mnaweza kuendelea na conversation bila muda wako kutawaliwa na calls.

  3. Mdiagnose kabla hujauza — elewa anahitaji nini na kwa nini amekutafuta.

  4. Usipitch, recommend — baada ya kuelewa shida yake, mpe recommendation inayolingana na situation yake.

  5. Tumia calls pale ambapo ni necessary — simu isiwe default ya kila customer.

Hii ndiyo aina ya biashara ninayotaka kujenga.

Biashara ambayo inaweza kuuza hata mimi nikiwa nafanya kitu kingine. Biashara ambayo mteja anaweza kunielewa, kuniamini na kununua bila kulazimika kuonana na mimi ana kwa ana.

Na kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi.

Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim)

Kama wewe ni Mjasi au Content Creator na uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni, jiunge kwenye community yetu kupata AI For Social Media Marketing Training:

Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital

Reply

or to participate.