- Elius' Letters
- Posts
- 173. Jinsi ya Kuuza Bila Kumfanya Mteja Ajisikie Anauziwa
173. Jinsi ya Kuuza Bila Kumfanya Mteja Ajisikie Anauziwa
Trust kubwa kwenye biashara haijengwi kwa kuuza kila mtu. Inajengwa kwa watu kuona kwamba unaelewa shida zao hata kabla hujafikiria pesa zao.
173. Jinsi ya Kuuza Bila Kumfanya Mteja Ajisikie Anauziwa
Kuna sentensi mbili ambazo zinaonekana zina maana moja, lakini kibiashara zina tofauti kubwa sana.
“Nimenunua gari.”
Na:
“Nimeuziwa gari.”
Mtu anayesema “nimenunua gari” anajisikia vizuri. Anaona amefanya uamuzi. Amechunguza, ameona kinachomfaa, akaamua kutumia pesa yake.
Lakini mtu akisema “nimeuziwa gari”, mara nyingi kuna hisia nyingine nyuma yake.
Anaweza kuanza kujiuliza kama alishawishiwa sana. Kama alipigwa bei. Kama alifanya uamuzi ambao asingefanya bila salesperson huyo.
Hapo ndipo biashara nyingi zinapokosea.
Tunafikiria kazi yetu ni kuwa wazuri sana kwenye kushawishi watu kununua.
Wakati mwingine, kadri unavyojaribu kushawishi zaidi, ndivyo mteja anavyozidi kujenga ukuta.
Kwa sababu binadamu wengi hawapendi kuuziwa.
Lakini tunapenda kununua.
Kwa hiyo kama unauza kupitia Instagram, WhatsApp, DM au content, skill muhimu sana si kujua jinsi ya kumpush mtu.
Ni kujua jinsi ya kumsaidia afikie uamuzi mwenyewe.
Kuwa Daktari, Sio Salesperson
Fikiria ukienda hospitali.
Daktari mzuri hakutazami sekunde tano halafu anaanza kukushawishi:
“Hii dawa ni nzuri sana. Watu wengi wanaitumia. Leo nina offer.”
Hapana.
Anaanza kwa kuuliza.
Unaumwa wapi?
Ilianza lini?
Una dalili gani?
Umetumia dawa gani?
Anafanya diagnosis.
Baada ya hapo ndipo recommendation yake inaanza kuwa na maana.
Hiyo ndiyo principle ambayo wafanyabiashara wengi tunaisahau.
Mteja akiingia DM na kuuliza:
“Bei gani?”
Tunajibu bei haraka.
Au tunaanza kutuma paragraphs za kwa nini bidhaa yetu ni nzuri.
Badala yake, jifunze kwanza kuelewa hali yake.
Kama unauza skincare, kabla ya kumpa bidhaa, elewa anachojaribu kutatua.
Kama unauza nyumba, elewa familia yake, budget, location anayohitaji na lifestyle yake.
Kama unauza consulting, elewa biashara yake iko wapi, imekwama wapi na anataka kufika wapi.
Hapa haujaribu kumteka mtu mpaka anunue.
Unajaribu kujibu swali moja:
Je, huyu mtu kweli anahitaji ninachouza?
Na ukifanya diagnosis vizuri, wakati mwingine jibu linaweza kuwa hapana.
Hilo nalo ni sawa.
Kwa sababu trust kubwa kwenye biashara haijengwi kwa kuuza kila mtu. Inajengwa kwa watu kuona kwamba unaelewa shida zao hata kabla hujafikiria pesa zao.
Usiuze Bidhaa, Uza Maisha Baada ya Bidhaa
Watu wengi wanajua bidhaa zao vizuri sana.
Wanajua material.
Wanajua model.
Wanajua features.
Wanajua specifications.
Tatizo ni kwamba mteja wako mara nyingi haamki asubuhi akiwa na hamu ya specification.
Anaamka akiwa na hamu ya matokeo.
Mtu anayenunua gari anaweza kuwa hataki tu engine nzuri.
Anataka kusafiri na familia yake bila stress.
Anataka gari lisilompa presha ya mafuta kila wiki.
Anataka akienda Moshi au Arusha ajisikie salama na familia yake.
Mtu anayenunua sofa si lazima awe obsessed na aina ya mbao iliyotumika.
Anaweza kuwa anataka sebule yake ionekane vizuri akipokea wageni.
Mtu anayenunua huduma yako ya social media marketing hataki posts 30 tu.
Anataka biashara yake ionekane, watu waulizie bidhaa, na mwisho pesa iingie.
Kwa hiyo unapouza, jiulize:
Baada ya kutumia bidhaa yangu, maisha ya huyu mtu yanabadilika vipi?
Hapo ndipo message yako inapaswa kuanzia.
Specifications zinaweza kuja baadaye.
Outcome ndiyo inayofanya mteja ajione ndani ya bidhaa.
Elimu Inafanya Nusu ya Selling Kabla Hujafungua DM
Mmoja wa wateja wazuri sana kumpata ni mteja ambaye tayari anaelewa.
Anaelewa shida yake.
Anaelewa kwa nini shida hiyo ni muhimu.
Anaelewa options zilizopo.
Na anaelewa kwa nini solution yako inaweza kumfaa.
Mteja wa aina hii hahitaji kuvutwa sana.
Ndiyo maana content ni muhimu sana.
Sio kwa sababu kila biashara lazima iwe influencer.
Content ni nafasi yako ya kufanya diagnosis kwa watu wengi kwa wakati mmoja.
Ni nafasi ya kuwasaidia waone shida ambazo walikuwa hawajazipa uzito.
Ni nafasi ya kuwaonyesha options.
Ni nafasi ya kuwafanya waelewe kile unachouza kabla hawajaingia WhatsApp yako.
Kama unauza saa, unaweza kufundisha jinsi ya kuchagua saa kulingana na mavazi au occasion.
Kama unauza magari, unaweza kufundisha kuhusu matumizi ya mafuta, maintenance, tofauti za models au jinsi ya kuchagua gari kulingana na matumizi.
Kama una salon, unaweza kufundisha clients jinsi ya kutunza nywele zao hata kabla hawajafika salon.
Kama wewe ni consultant, fundisha watu jinsi ya kutambua tatizo kabla hawajahitaji consultant.
Hapo ndipo content inaanza kufanya kazi kama salesperson ambaye yuko kazini hata wewe ukiwa umelala.
Na ndiyo maana content nzuri haiishii kusema:
“Tunauza hii.”
Inasema:
“Hii ndiyo shida.”
“Hivi ndivyo inavyokuathiri.”
“Hivi ndivyo watu wengi wanavyokosea.”
“Na hizi ndizo options zako.”
Mteja akiingia kwenye DM baada ya kupitia elimu hiyo, mazungumzo yenu yanaanzia mbele zaidi.
Si stranger tena.
Ana context.
Fanya Ofa Yako Iwe Hatua Inayofuata Kawaida
Hii ndiyo sehemu ninayoipenda zaidi.
Selling nzuri haipaswi kujisikia kama kuruka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine bila sababu.
Inapaswa kuwa na flow.
Fikiria dalali wa nyumba amekutana na mtu mwenye familia kubwa.
Anauliza:
Mko watu wangapi nyumbani?
Budget yako ni kiasi gani?
Unataka kuwa karibu na mjini?
Unataka bedrooms ngapi?
Unafanya kazi upande gani wa Dar?
Baada ya majibu hayo, akisema:
“Kwa maelezo yako, hizi nyumba tatu Mikocheni na Masaki ndizo zinaonekana kukufaa zaidi.”
Recommendation hiyo haijisikii kama sales pitch.
Inajisikia logical.
Mteja mwenyewe anaona kwa nini nyumba hizo zimefika mezani.
Hicho ndicho unachotaka kujenga kwenye biashara yako.
Diagnose kwanza. Elewa tatizo, mazingira na kile mteja anachotaka.
Onyesha outcome. Msaidie aone anakoenda baada ya tatizo kutatuliwa.
Muelimishe. Mpe context ya kuelewa options zake.
Present offer kama next logical step. Sio kitu kilichotokea ghafla kwa sababu sasa unataka pesa.
Lakini bado kuna hatua moja muhimu.
Mwache achague.
Unaweza kusema:
“Kwa kile ulichonieleza, hizi option mbili ndizo zinazokufaa zaidi. Kati ya hizi, ipi unaona inakufaa?”
Mteja akichagua, anamiliki uamuzi wake.
Hilo ni tofauti sana na kusema:
“Chukua hii. Hii ndiyo best.”
Unapotaka kumcontrol sana mteja, resistance inaongezeka.
Unapompa clarity ya kufanya uamuzi, confidence inaongezeka.
Content Yako Inaweza Kufanya Haya Yote
Hivi vitu havitumiki kwenye calls pekee.
Unaweza kufanya diagnosis kupitia content.
Unaweza kuuza outcome kupitia content.
Unaweza kuelimisha kupitia content.
Unaweza kufanya offer ionekane kama next logical step kupitia content.
Unaweza kumpa mteja options kupitia content.
Hapo ndipo social media inaanza kutoka kuwa sehemu ya kupost picha na kuwa mfumo wa mauzo.
Badala ya kila siku kuamka na kusema:
“Leo nipost nini?”
Unaanza kuuliza:
“Mteja wangu anahitaji kuelewa nini ili afanye uamuzi mzuri?”
Hilo ni swali tofauti kabisa.
Na ndiyo maana mtu mwenye followers wachache lakini ana audience iliyo informed anaweza kuwa na biashara nzuri kuliko mtu mwenye followers wengi lakini hakuna anayeelewa anachouza. Mfumo wa positioning, content, conversion na follow-up ndiyo unaamua kama attention hiyo itageuka kuwa biashara, sio follower count pekee.
Kama unauza kupitia Instagram na WhatsApp na unataka kujenga hii process kwa kutumia AI, nimeweka mfumo huu ndani ya Tumia AI Kuuza Online — tumia.zillim.digital — kuanzia positioning na content mpaka mazungumzo yanayogeuza interest kuwa mauzo.
Mteja Hahitaji Kushindwa na Wewe, Anahitaji Kufikia Uamuzi
Acha kushawishi kila mtu; diagnose kwanza kama kuna shida unayoweza kutatua.
Usieleze bidhaa tu; onyesha matokeo ambayo mteja anataka kuyapata.
Elimisha kabla ya kuuza ili mteja aingie kwenye mazungumzo akiwa tayari anaelewa.
Fanya bidhaa au huduma yako iwe hatua inayofuata kwa sababu ya diagnosis, sio kwa sababu umeamua kupush offer.
Mpe mteja nafasi ya kuchagua ili ajisikie amefanya uamuzi, sio amelazimishwa kufanya uamuzi.
Ukianza kufanya hivi, selling inaanza kuwa nyepesi zaidi.
Sio kwa sababu umejifunza ujanja wa kucontrol watu.
Ni kwa sababu umeacha kujaribu kucontrol watu.
Unaanza kuwasaidia kuelewa.
Unaanza kuwaongoza.
Unaanza kuwapa clarity.
Na mwisho, mtu sahihi akiona kwamba unachouza kinaendana na shida yake na matokeo anayoyataka, kununua kunakuwa uamuzi wa kawaida.
Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Chagua moja kati ya hizi principle tano na uitumie kwenye content au mazungumzo yako ya WhatsApp wiki hii.
Na kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia AI kukuza biashara yako ya mitandaoni — jiunge kwenye community yetu kupata AI For Social Media Marketing Training:
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply