• Elius' Letters
  • Posts
  • 168. Hauhitaji Kwenda Viral Ili Uuze Online (Tumia AI Step by Step)

168. Hauhitaji Kwenda Viral Ili Uuze Online (Tumia AI Step by Step)

Mauzo yanatokana na mfumo. Mfumo rahisi. Mfumo simple ambao unaweza ukatumia AI kuutengeneza sasa hivi. Na kazi ya huu mfumo ni kuziba mapengo makubwa manne ambayo unayakuta kwenye biashara. Nitakuelezea kuhusu haya mapengo hivi punde.

Letter 168. Hauhitaji Kwenda Viral Ili Uuze Online

Kama umekuwa ukijitangaza kwenye mitandao ya kijamii, utagundua kwamba hauhitaji kwenda viral.

Unachohitaji ni mfumo ambao unaweza ukauendesha ndani ya dakika 30 kwa siku. Mfumo ambao unakuletea mauzo. Unaweza kuwa na mfumo ambao unakuletea mauzo hata siku ambazo uko busy, siku ambazo umetingwa na kazi, siku ambazo wateja wanaonekana wako slow, bado mfumo wako inabidi ufanye kazi.

Kama huo mfumo hauna, inaweza ikawa vigumu sana wewe kuuza. Unaweza ukajikuta unakaa kwenye pedestal ambayo kila mwezi ukifika unakuwa hauna uhakika unatengeneza kiasi gani cha pesa. Hauna uhakika na mauzo yako. Hauna uhakika na wateja. Hiyo ni kwa sababu tu unakosa mfumo ambao unaweza ukauendesha ndani ya nusu saa kwa siku.

Mauzo ya uhakika hayatokani na followers

Mauzo ya uhakika hayatokani na followers. Na uhakika hiki kitu unakifahamu.

Kuna watu wana followers wengi sana, lakini hawauzi zaidi. Kuna biashara zimeanza na followers sifuri, lakini kwa sababu ya mfumo wa kujitangaza zimeweza kukusanya followers wengi na kuanza kuuza. Kitu kimoja ambacho nimejifunza ni kwamba hauhitaji kuwa na followers wengi, hauhitaji kwenda viral, na hauhitaji kupost zaidi.

Huhitaji kusema kwamba inabidi upost mara nyingi ili uweze kuuza.

Mauzo yanatokana na mfumo. Mfumo rahisi. Mfumo simple ambao unaweza ukatumia AI kuutengeneza sasa hivi. Na kazi ya huu mfumo ni kuziba mapengo makubwa manne ambayo unayakuta kwenye biashara. Nitakuelezea kuhusu haya mapengo hivi punde.

Biashara nyingi zina mapengo makubwa manne. Na haya mapengo usipoyaziba kwenye biashara yako, unaweza ukajikuta hata ukiongeza bajeti ya matangazo ya kulipia hauuzi zaidi. Hata ukiongeza idadi ya content unazopost kila siku hauuzi zaidi. Hata ukiongeza followers hauuzi zaidi.

Kwa sababu tu unakosa mfumo ambao unaziba yale mapengo. Okay, lets talk about those pengos my friend…

Positioning: watu waone wewe ni tofauti

Pengo la kwanza tunaliita positioning.

Positioning ni kitendo cha kuhakikisha kwamba biashara yako inavyoonekana, kwa namna yoyote ile ambavyo watu wanaiona kwenye mitandao ya kijamii au popote pale wanapoiona, mtu aweze kujua kabisa kwamba huyu mtu ni tofauti na watu wengine wote. Tulia sasa ikuingie, umeelewa nilichosema hapo? Hata tofauti ndogo inaweza kukusaidia kujiposition vizuri na ukauza kuliko washindani.

Sio mtu anaangalia akaunti yako Instagram, TikTok au Facebook, anaona kama biashara yako inafanana na biashara za watu wengine 5,000 ambao ni washindani wako.

Inabidi utafute namna hata ya mwonekano kwenye biashara yako unatofautiana kabisa na watu wengine wote ambao wanafanya biashara kama ya kwako. Inaweza kuwa speed ya delivery, inaweza kuwa aina ya wateja unaohudumia au inaweza kuwa hata style unayotumia. Hiyo ndio positioning.

Mfano, ukiwafuatilia CFEs wa tanzania, utagundua ni wengi sana kama mchwa, lakini waliofanikiwa ni wale waliojiposition, unakuta mmoja anaongelea retirement, mwingine uwekezaji katika hisa, mwingine jinsi ya kuweka budget, mwingine anaongelea utt tu… hyo ni strategy. inawasaidia kuattract specific clients na wanatengeneza pesa kuliko kama wote wangeimba kwaya. Sijui umenipata?

Unajiweka kwa namna ambayo watu wanaona kama wewe ni tofauti na watu wengine wote. Hii nimeielezea sana kwenye masterclass na nimekuonesha kabisa jinsi ya kutumia ai kuunda a very unique positioning.

Content Strategy: usipost kwa mood

Pengo la pili tunaita content strategy.

Content strategy ni mbinu yako ya content. Jinsi unavyojitangaza. Lakini aina ya content unazotengeneza zinaweza zikavutia watu sahihi au zikawafukuza hao watu sahihi.

Kwa hiyo usipost kwa mood.

Sio kwamba inabidi uamke asubuhi useme, “leo najisikia kupost hiki.” Hapana my friend.

Inabidi uwe na mpangilio wa content ambazo hata siku ambayo unaumwa, hata siku ambayo hujiskii kabisa kabisa kutembea, bado kuna content unaweza ukatengeneza ambazo zinakuletea matokeo.

Hata kama hyo siku unaenda kujifungua, usikose content za kupost. I remember six months ago, business partner wangu ambaye pia ni dada yangu @pregnancy_nutritiontz mwenye 200k+ followers across social media, alikuwa labour… kwa wale ambao hamjui leba ni nini, inamaanisha ulivyozaliwa mama yako hyo siku alikuwa sehemu wodini na manesi, wanamwambia push, pusshh… na hapa siongelei constipation. Naongelea kuleta binadamu duniani. Its a godly situation.

Lakini hata siku hyo akiwa kitandani alikuwa anapost bidhaa zake na huduma zake na kujitangaza online. I was very amazed kwakweli na mara nyingi ninapojisikia uvivu kupost hii scenario inanikumbusha kuwa serious.

Inanikumbusha kuwa Its part of your life wewe kama mjasi. Technolojia kurahisishia hii process na kuacha uvivu na perfectionism ili ujitangaze bila kupoteza muda online.

Shida ni moja. Ukipost kwa mood, kwamba leo unapost kesho haupost, baada ya wiki algorithm inakusahau. Na algorithm ikikusahau, engagement yako inashuka, views zako zinashuka, na hiyo inaathiri sana biashara yako. Sasa kuna aina ya content ambazo ni rahisi kutengeneza na kupozt ndani ya dakika moja, kila biashara ina aina yake, kwahyo dont hesitate kujaribu vitu vipya hasa ninavyokufundisha.

Tuendelee, maana naona unaanza kusinzia.

Conversion: Usifocus kwenye views nyingi, pima ni watu wangapi wananunua.

Pengo la tatu tunaliita conversion.

Conversion inaweza ikaonekana kama ni maneno magumu, lakini usiwe na wasiwasi. Conversion ni kipimo cha watu wangapi walioona content zako wamenunua. Au ni wangapi kati ya waliokutafuta DM wamenunua.

Kama watu wanaona content zako 1,000 alafu hupati hata mteja mmoja, maana yake conversion ni sifuri. Kama watu 100 wanaona content zako na wananunua watu 10, maana yake una conversion rate ya 10%. Hongera sana.

Kwa hiyo lengo lako sio kuwa kwenye average.

Lengo sio kupata views nyingi. Lengo ni kuongeza wingi wa watu wanaoshawishika pale wanapoona content zako. Tafadhali naomba usome tena hii sentensi. Au, ngoja niiandike tena hapa, kwani kuna shida gani, hii si ndo injili yangu? Huu si ndo walaka wangu kwako? Nimesema…

“Lengo sio kupata views nyingi. Lengo ni kuongeza wingi wa watu wanaoshawishika pale wanapoona content zako.”

Lazima uwe na mfumo ambao unabadilisha watu wanaoona content zako kuwa wateja wako. Bila huo mfumo unaweza ukajikuta unapost zaidi lakini hauuzi.

Fikiria mfano huu hapa. Unauza bidhaa 50k tsh, Unapata message 500 kwa mwezi au kwa wiki. Unauza bidhaa za lishe au ni coach, or whatever. Kati ya watu 500 wanaokutafuta, ni 50 tu ndio wananunua. Hyo ni 10% conversion. Ni asilimia kumi tu, na hii ni very common kwa watu wanaotengeneza matangazo ya kulipia. Unapata message 10, lakini wanaonunua ni mmoja. Meaning unatengeneza 2.5M.

Sasa fikiria kama ulikuwa na mfumo ambao unakuongezea conversion kutoka 10% mpaka 25%. Followers ni wale wale. Bajeti yako ya matangazo ni ile ile. Lakini idadi ya watu 500 kati yao wanaobadilika kuwa wateja inaongezeka kwenda 125. Umeuza 6.25M tsh. Unaona sasa hapo tajiri?

Hii ndio nguvu ya mfumo.

Unachohitaji sio kupost zaidi, sio kutengeneza content zaidi, sio kucheza zaidi na kujisnap dukani wako kama sugarbaby, na sio kuongeza bajeti yako ya matangazo. Ni mfumo unaongeza efficiency ya kile kinachofanya kazi tayari.

Sema, leo nimekupa nondo kubabeki. Twende pengo la mwisho sasa.

Retention: usipoteze wateja unaowapata

Pengo la mwisho tunaliita retention.

Retention ni kama kasayansi fulani hivi, kambinu kako mwenyewe ka kutunza wateja wako. Kama ukipata wateja unawapoteza, utajikuta kila siku unalazimika kujitangaza upya.

Kila siku unalazimika kujitangaza upya kwa sababu lengo la biashara ni kukusanya wateja na kuwatunza, na wewe huna mfumo wa retention.

Kama wewe kila unapopata mteja unampoteza, maana yake utalazimika kujitangaza kila siku. Na hiyo inaweza kufanya biashara yako iwe kama gereza lako.

Nakumbuka Client wangu mmoja anaitwa Dr Aurelia (@healthyliving_with_draurelia 80.3k followers) ambaye tulianza akiwa na followers 5000. Kila week aikuwa analipia zaidi ya laki 3 kwenye matangazo na bado hapati wateja, asipolipia matangazo kwa mwezi mzima alikuwa anapata views 800 tu organic. Sasa hivi mambo yamebadilika, sio kila homa ni malaria… anasema anapata wateja na views 4+M organic views bila hata kulipia matangazo

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini kuna wakati unaweza kurudi sehemu ambazo uliwahi kwenda, kama mimi nimesoma SUA Morogoro au nyumbani Bukoba, na kukuta vitu ulivyoviacha ndio viko hivyo hata kama uliondoka miaka mitano iliyopita?

Hiyo ni kwa sababu watu wengi wanaendesha biashara kwa mazoea. Kwa namna ile ile. Kwa sababu tu huyu mwingine anafanya hivi, na yeye anafanya hivyo hivyo.

Hupasi kuendesha biashara yako hivyo. Ukiendesha biashara yako kama ulivyozoea, utapata matokeo uliyozoea. Jitoe kwenye hyo confort zone, jufunze then utapata effortless growth baada ya kuweka efforts za kutosha.

Leo nadhani umeenjoy barua yangu. Ngoja nikukumbushe maana kwa wewe utakayejiunga na sisi kwenye Tumia AI Kuuza Online Masterclass this week utaondoka na mfumo wako wa kuendesha biashara yako in 30 minutes kwa kutumia AI. Mfumo huo huo wanaotumia wanafunzi wangu utaweza kujenga wa kwako ambao unaiposition biashara yako kwa utofauti, unatengeneza content ambazo ni unique, unaconvert wateja zaidi na kuwatunza. Huu mfumo unaweza kuuendesha ndani ya dakika 30 tu kwa siku.

Mfumo wa AI wa kuuza online

Ukiwa na mfumo wa AI wa kuuza online, unajenga vitu vikubwa vinne.

  1. Unajenga AI Powered Business Profile ambayo inatengeneza context ya biashara yako na foundation ya biashara yako, ili AI yoyote aweze kukuelewa na kukusaidia. Huu ndo mwanzo wa positioning.

  2. Unatengeneza content ambazo zinafanya kazi tatu: kuwaelimisha wateja wako, kujenga trust, na kuwauzia ili wasikusumbue DM na maswali bila kununua. Hii ndo itakuwa strategy yako ya content.

  3. Unatengeneza WhatsApp sales flow system ambayo inabadilisha watu wanaokutafuta kutoka DMs au WhatsApp kuwa wateja, huu ndo mfumo wa conversion.

  4. Unatengeneza follow-up system ambayo inakusaidia kutunza wateja na kubadilisha asilimia kubwa ya watu waliokutafuta wawe wateja. Mfumo wa kuwatunza na kuwafuatilia wateja wako.

Nasisitiza uzuri wa huu mfumo ni kwamba unaweza ukauendesha ndani ya dakika 30 kwa siku.

Na ndani ya masterclass ya “Tumia AI Kuuza Online,” unaweza kutengeneza misingi ya biashara yako, mfumo wa content, mfumo wa mauzo, na mfumo ambao unaurudia kila siku.

Sio kila mfanyabiashara anafaa kuingia kwenye hili darasa. Linafaa kama tayari una biashara, unafanya mauzo, lakini unapata message nyingi za wateja wanaoulizia bei alafu hawanunui.

Linafaa kama una biashara tayari, lakini haujaweka mifumo vizuri. Hauna mpango. Hauna strategy ya kujitangaza. Mara nyingi unajiuliza, “leo nipost nini?”

Linafaa kama una biashara na unataka mfumo wa mauzo. Sio kozi ya miezi miwili au mitatu ambayo itakupotezea muda mwisho wa siku haufanyi kitu cha maana.

Lakini kama haujajua unauza nini, haujaelewa wateja wako, hauna mpango wowote na unatafuta njia ya haraka ya kutengeneza pesa, hii sio kwa ajili yako. Ni bora uje uanze na darasa letu la 30 Days 30-Days Social Media Business Starter Program ambayo ina madarasa 30 ya kukusaidia kuanza kama beginner.

Mfumo ndio unaongeza mauzo, sio kelele za mitandaoni.

  1. Hauhitaji kwenda viral; unahitaji mfumo ambao unaweza kuuendesha ndani ya dakika 30 kwa siku.

  2. Mauzo ya uhakika hayatokani na followers; yanatokana na mfumo unaoziba mapengo hayo manne ya biashara.

  3. Positioning inafanya watu waone wewe ni tofauti na washindani wako wote.

  4. Content strategy inakusaidia usipost kwa mood, bali upost content zinazovutia watu sahihi.

  5. Conversion inabadilisha watu wanaoona content zako kuwa wateja.

  6. Retention inakusaidia kutunza wateja ili biashara yako isiwe gereza lako.

Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim)

Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi. Jiunge na Tumia AI Kuuza Online Masterclass

Ada ni tsh 199,500/= tu baadala ya 500,000/=

Fanya Malipo 0760962379 Jina Elius Kamuhangire (Mpesa au Selcom Bank) Kisha

Nitumie message whatsapp tuaze na Darasa.

Click kunitext whatsapp hapa +255760962379

Elius Kamuhangire McBenvics
Mjasi | Creator ZillimDigital

Reply

or to participate.