- Elius' Letters
- Posts
- 051. Jinsi ya Kuchagua Mwelekeo Mmoja wa Biashara Unaotumia AI (na Kuacha Kuanza Upya Kila Mara)
051. Jinsi ya Kuchagua Mwelekeo Mmoja wa Biashara Unaotumia AI (na Kuacha Kuanza Upya Kila Mara)
Elius Letters — Mwelekeo mmoja kwa siku 90
001. Jinsi ya Kuchagua Mwelekeo Mmoja wa Biashara Unaotumia AI (na Kuacha Kuanza Upya Kila Mara)
Kuna mtu aliniambia juzi: "Nimejaribu kuagiza mizigo china, kisha nikaanza coaching, kisha kuuza nguo online, kisha ulivyonifundisha AI sasa hivi naanza kuwaandikia matangazo wateja lakini hakuna kinacholipa vizuri." Jamaa alikuwa amechoka. Sasa sio kwamba hana akili, hapana ana akili nyingi tu,na hilo ndo tatizo, kila akili inataka njia yake.
Hii ndiyo hali ya Wajasi wengi. Unafanya vitu vingi. Unajifunza kila wiki. Unapost. Unajibu DM. Unabadilisha bio. Unasikia podcast mpya inaogelea fursa mpya, unasema "ah, hii sasa ndo yenyewe!" kisha mwezi ujao uko kwenye kitu kingine kabisa. Hela inakuja mara kwa mara, kisha inaisha. Na unajiuliza: je, tatizo ni mimi?
La hasha, Tatizo ni ukosefu wa mwelekeo mmoja na mfumo mmoja unaounga mkono mwelekeo huo.
Kwa Nini Wazo Jipya Halileti Pesa
Kila unapobadilisha mwelekeo wako, unarudi hatua za mwanzo. Unajenga audience mpya. Unajifunza lugha mpya ya soko lako. Unatengeneza offer mpya. Unaanza kutengeneza uaminifu kutoka zero. Hii inaitwa "kuanza upya" na ni expensive kuliko unavyodhani.
Fikiria kwamfano ungekuwa wewe ni kibanda cha biashara yako mtaani hapo ina maana kila wiki unabadilisha bidhaa: leo chipsi, kesho nguo, kesho kutwa simu. Mteja anapita mara moja, anasema "ah, huyu hajui anauza nini," na haendi tena. Soko halijui unasimama wapi na wewe mwenyewe hujui.
Wazo jipya huonekana kama true freedom. Lakini kiuhalisia ni mzigo. Kwa sababu huwezi kujenga mfumo juu ya kitu kinachobadilika kila mwezi. Mfumo unahitaji msingi, foundation. na msingi unahitaji mwelekeo mmoja.
Mwelekeo Mmoja, Mfumo Mmoja
Mwelekeo sio kufanya biashara inayouza vitu expensive. Mwelekeo ni jibu la swali moja: "Ninamsaidia nani, kwa nini, na kwa njia gani?"
Sio "nauza kwa mtu yeyote." Sio "nafanya kila kitu kinachoniingizia pesa." Ni mwelekeo mmoja, mtu mmoja unayemsaidia, tatizo moja unalosuluhisha, na njia moja unayoitumia kufikia huyo mtu.
Mfano: mtu anayejua kupika vizuri anaweza kuwa na mwelekeo "kuwasaidia wanawake wanaouza chakula kwenye Instagram kuandika matangazo yanayouza kwa AI." Hiyo sasa ni mwelekeo. Sio "nafanya kila kitu na AI." Sio "nauza chakula na pia nafundisha na pia nafanya design." Direction ni moja.
Mfumo sasa ni kile unachofanya kila wiki ndani ya mwelekeo huo huo: content, DM, follow-up, bei. Bila mwelekeo, mfumo hauna mahali pa kusimama.
Assignment nayokupa wiki hii: Andika sentensi moja: "Ninamsaidia [mtu fulani] kufanya [matokeo fulani] kwa kutumia [njia yako]." Usiifanye iwe perfect sasa, wewe andika tu. Hiyo sentensi ndiyo mwelekeo wako wa muda sio ahadi ya maisha yako yote, ni msingi wa siku 90 zijazo.
Sheria ya Siku 90
Kuna sababu watu wengi hubadilisha mwelekeo kabla wa kuona matokeo: matokeo hayaji kwa wiki mbili. Yanakuja baada ya kurudia kitu kimoja kwa muda mrefu.
Siku 90 sio adhabu. Ni majaribio. Unachagua mwelekeo mmoja, unasema "kwa miezi mitatu, nitafanya hivi tu" na unapima. Unapost kuhusu hilo. Unazungumza na watu kuhusu hilo. Unajaribu kuuza kitu ndani ya hilo. Baada ya siku 90, una data za kutosha. Unajua kama mwelekeo unaishi au hautoishi kwa sababu umejaribu, sio kwa sababu uliogopa.
Mtu mmoja namfahamu alibadilisha biashara mara nne kwa mwaka. Mwaka mzima ukaisha, alikuwa na followers 2,000 na mauzo ya TZS 0. Mwaka uliofuata alichagua biashara moja tu kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kuandika WhatsApp messages zinazofunga mauzo. Baada ya siku 90, alikuwa na wateja kumi na watatu wanaolipa. Sasa sio kwa sababu alikuwa na bahati, hapana. Ni kwa sababu alisimama mahali pamoja kwa muda mrefu vyakutosha kusikika na soko.
Assignment ya wiki hii: Weka kalenda yako leo hadi siku 90 zijazo. Andika mwelekeo wako juu ya kalenda yako. Kila unapoona wazo jipya linalovutia, usilifuate. Andika tu kwenye daftari: "Baada ya siku 90." Hiyo ndiyo nidhamu ya mwelekeo.
Wengi wanadhani lazima wawe na ujuzi special kabla ya kuchagua mwelekeo. "Sijui coding." "Sina degree." "Najua tu vitu vya kawaida." “Sijui kutengeneza content“ “Sijui Maswala ya IT“
Lakini kile unachokijua ambacho ni kawaida kwako kinaweza kuwa kitu kinachokosekana kwa mtu mwingine. Mjasi anayejua jinsi ya kupost kwenye Instagram kila siku, hata bila followers wengi, ana ujuzi ambao mtu anayeanza leo hana. Mjasi anayejua jinsi ya kujibu DM bila kukata tamaa ana ujuzi ambao mtu anayechukia WhatsApp sales anahitaji.
AI haizidi ujuzi wako. AI inaongeza kwenye ujuzi wako na inakufanya uonekane na kufanya kazi kama mtu mkubwa zaidi. Lakini lazima ujue unachotoa kwanza. Mwelekeo unatoka kwenye kile unachokijua tayari, siyo kwenye kitu unachosikia kinatrend leo.
Fikiria, tuseme mfano unauza viazi kwenye soko. Viazi ni kitu cha kawaida. Lakini wewe unajua wapi viazi vizuri, unajua bei, unajua wateja wanapenda vipi. Hiyo "kawaida" ndiyo biashara yako — ukiiweka kwenye mfumo.
Assignment ya wiki hii: Andika orodha ya vitu 5 unavyojua vizuri hata vitu vidogo. Kisha andika: "Nani anaweza kulipa kwa hili?" Kama tulivyofanya kwenye assignments za nyuma usitafute jibu perfect kwanza. Tafuta mtu mmoja tu.
sasa Tuongelee AI.
AI ni kama Msaidizi wa Uamuzi, Sio Chimbuko la Mawazo
Watu wengi wanatumia AI kuzalisha mawazo 50 kisha wanakwama tu wakiwa na mawazo yao 50 zaidi ya hapo awali. Hiyo sio AI inayosaidia. Hiyo ni AI inayozidisha mizozo kichwani.
Sasa nataka nikupe njia tofauti, tumia AI kuchuja, sio kuzalisha zaidi. Mpe AI profile yako ujuzi wako, muda wako, kile unachopenda kufanya, kile unachotaka kupata. Kisha muulize: "Nipe mielekeo mitatu tu ya biashara inayofaa kwa profile hii. Pendekeza mmoja." Hiyo ndiyo AI inavyofanya kazi vizuri, inakusaidia kuchagua, sio kuanza upya.
Generic in, generic out.
Ukimpa AI "nataka kufanya biashara online," atakupa majibu ya kawaida sana. Lakini ukimpa AI ukweli wako, mfano "najua kupika, nina muda wa masaa 2 kwa siku, napenda Instagram, nataka TZS 500,000 kwa mwezi" atakupa mwelekeo unaoweza kujaribu.
Sasa naomba tuelewane hapa, AI sio mwelekeo wako. AI ni msaidizi wa kuamua mwelekeo. Uamuzi bado ni wako ndugu yangu. Na uamuzi huo unahitaji kujaribiwa kwa siku 90, si kwa saa 2. This is very important. Nimeandika hii nikiwa natamani sana unielewe maana ukiichukulia poa, muda utafika ambao utatamani ungenisikiliza na kuanza.
Okay, ngoja nikupe assignment nyingine hapa, na ole wako usizifanye.
Assignment wiki hii: Andika profile yako kwa sentensi 5 ujuzi, muda, kile unachopenda, kile unachohitaji kama kipato. Tumia AI kuuliza mwelekeo options 3. Chagua mmoja. Andika sentensi ya mwelekeo. Usifanye kitu kingine kwa wiki hii, jaribu huo mwelekeo tu.
Ujumbe Mkuu wa Barua yangu ya leo: Moja Ndiyo Inakutosha
Mwisho wa siku, tatizo sio ukosefu wa mawazo. Tatizo ni ukosefu wa kujitolea kufuata direction moja
1. Mwelekeo mmoja unaruhusu mfumo mmoja na mfumo ndio unaolipa.
2. Siku 90 ni muda wa majaribio, si kifungo cha maisha.
3. Ujuzi wako wa "kawaida" unaweza kuwa msingi wa offer inayolipiwa na wateja.
4. Tumia AI kuchagua, si kuzalisha mkanganyiko zaidi.
Usisubiri kujua kila kitu kabla ya kuchagua. Chagua, jaribu kwa siku 90, kisha rekebisha kwa data si kwa hofu.
Jifunze Kujitangaza Online na AI (na Zillim Growth Club)
Kama umejifunza kitu leo, usiishie kusoma tu. Fanya mazoezi.
Na kama wewe ni Mjasi au Content Creator uko tayari kujifunza zaidi kuhusu kutumia
AI kukuza biashara yako ya mitandaoni jiunge kwenye group letu kupata
Madarasa yatakayokusaidia kuanzisha na kutengeneza mfumo wako wa kuuza online
Ndani ya hili darasa utaondoka ukiwa na mfumo mzima ambao utatumia kuendesha biashara yako nzima kwa AI in 30 minutes a day.
Ada ni tsh 199,500/= tu baadala ya 500,000/=
Fanya Malipo 0760962379 Jina Elius Kamuhangire (Mpesa au Selcom Bank) Kisha
Nitumie message whatsapp tuaze na Darasa
Click kunitext whatsapp hapa +255760962379
Elius Kamuhangire
Mjasi | Creator ZillimDigital
Reply